HALMASHAURI ya wilaya ya Njombe utafitu umebaini kuwa kila
wanapo kutana watu 100 watu 15 wameambukizwa virusi vya ugonjwa wa ukimwi huku
kila penye kundi la watu 100 watu 12 wamepima maambukizi ya virusi vya ukimwi
hali ambayo inaashilia kuwa maambukizi yanazidi kuongezeka kila siku.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Njombe kwenye kikao
cha kupambana na maambukizi ya virusi vya ukimwi kilicho wakutanisha viongozi
wa halmashauri hiyo na viongozi wa madhehebu ya dini ili kutafta namna ya
kuwanusuru wananchi na waumini na ugonjwa huo.
Dumba alisema kuwa katika halmashauri ya mji wa Njombe
takwimu zinaonyesha kuwa maambukizi ya virusi yanakua kwa kasi katika kundi la vijana na akina mama ambao wamekuwa
wakibainika wakati wa kupimwa wakiwa na ujauzito.
Ametoa wito kwa wakina mama wajawazito kuendelea kujitokeza
kupima ili kupata huduma ya kuwakinga watoto ambao hawajazaliwa kupata
maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa kuanza kutumia dawa za kinga.
Naye mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe, Iluminata Mwenda alinyesha kusiktishwa na hali ya
maambukizi ya Ukimwi katika halmashauri ya hiyo na kueleza kuwa hilo pigo
linalo sababisha maendeleo ya wakazi hao kudumaa kutokana na vingozi na wadau wengine kutumia
muda mwingi pamoja na rasilimali fedha kutafta namna ya kupambana na Ukimwi.
Hivyo aliwataka viongozi wa Dini kuhakikisha wanatoa elimu
kwa waumini wao kwani watu wanao gundulika na maambu kizi wengi ao ni waumini
na kuwa elimu ikitolewa kikamilifu wananchi wakatamua kuwa matumizi sahihi ya
kinga na kujua namna ya kujikinga kwa kuwa na mpenzi mmoja ambapo wanahinizwa
kuoa na kutulizana.
Kwa upandewa viongozi wa dini walio kuwepo katika mkutano
huo waliiomba selikali kutoa elimu ya kutumia kinga vizuri na wao watafanya
kazi ya kuweka hofu ya Mungu kwa waumini wao kutoka katika dini mbalimbali.
Mchungaji Bernard Sagaya alisema kwa upande wa serikali
ifanyemajukumu yake ya kutoa elimu kwa wananchi na kuwa anawaomba viongozi wa
serikali kujitokeza katika mikutano ya dini ili kukazia masomo yanayotolewa na
viongozi hao katika mikutano yao mbalimbali na katika makanisa ili kufikia
malengo ya kutokomeza Ukimwi
Mratibu wa Ukimwi halmashauri ya mji wa Njombe Daniel Mwasongwe
alisema ameeleza changamoto zinazoyakabili mapambano dhidi ya Ukimwi na
mikakati iliyopo kueneleza mapambano kuwa ni pamoja na kutokomeza maambukizi
kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto