ZAIDI ya milioni 10.8 zimeokolewa na Taasisi ya Kupambana na
Kuzuia Rushwa (Takukuru) mkoani Njombe, kwa mwaka huu katika taasisi mbalimbali
kwenye miradi ya maendeleo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa Takukuru
mkoa wa Njombe Charles Nakembetwa alisema kuwa taasisi hiyo imefanikiwa
kuziokoma pesa hizo zikiwa katika hatari ya kuchomolewa katika miradi ya
kimaendeleo katika taasisi mbalimbali za serikali.
Nakembetwa alisema kuwa taasisi hiyo imeziokoa jumla ya
shilingi 10,864,000 ambapo takukurui walipata taarifa kutoka kwa watu na
kuzifanyia kazi na kuzuia kutolewa kama rushwa katika miradi ya kimaendeleo
mkoani hapo.
Alisema kuwa Takukuru kwa sasa imekuwa ikitumia mfumo wa
kuhakikisha wanazuia rushwa kabla ya kutokea na pesa kutumia vibaya kitu
kinachookoa pesa, kuliko kusubili rushwa itolewa na kumkamata mtuhumiwa ambapo
akikamatwa uwezekano wa kupatikana kwa pesa hizo unakuwa ni mgumu.
Alisema udhibiti huo wa mianya ya kutoa rushwa kuna saidia
kuokoa pesa za serikali kutumika vibaya kutokana na kutoa ama kupokea Rushwa
wakati wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya serikali.
Nakembetwa alisema kuwa kwa mkoa wa Njombe kwa sasa kuna
kesi 28 ambazi zipo mahakamani na kuwa kwa mwaka huu wamefungua kesi 5 na kuwa
kuna kesi ambazo zinatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni.