Huu ndio Msaada wa sheria kuhusu bima


Kiukweli mimi nimesononeshwa sana na hili shirika kwanza kabisa nashindwa kuelewa
wanatuchukuliaje sisi watumishi wa chini kabisa.

Kuna kipindi huwa nafikia hatua ya kuwachukulia kama wezi wa kisasa mfano mzuri kwa watumishi
Kuna huduma ya BIMA YA MAISHA (Bima ya matumaini) watumishi wengi wananyanyasika na
hili niliweke wazi ni kutokana na maisha yao kuwa magumu imefikia hatua ndo imekuwa kilio kwao
wanawashawishi watu wajiunge kwenye huduma hizo kwa lengo la kujiwekea fedha kidogo kidogo
kwa muda wa miaka 3 halafu unapewa asilimia 20 ya pesa yako itakayokatwa kwa miaka 9 lakini cha ajabu miaka mitatu inaweza kufika ukazunguushwa mpaka miezi isiyojulikana na wakat huo mtu anategemea kuipata hiyo pesa kwa ajili ya mipango aliyojiwekea mfano mimi na kaka yangu
mtumishi mkoani simiyu hukoo vijijini alipaswa kulipwa fedha yake tangu june lakini mpaka sasa
hajalipwa pesa na ameshasafir kwenda kwenye ofisi zao zaid ya mara tatu na istoshe gharama ya
nauli ni sh 23000 kwenda tuuu ukizidisha kiasi alichotumia kufuatilia pesa yake ni nusu ya pesa
anayopaswa kulipwa na hajalipwa mpaka sasa na alishamtumia mkurugenzi wa shirika e-mail lakini
haikujibiwa Mi niwaombe NIC mjaribu kutuhurumia wenzeni tunaotumia viatu vyenye soli zilizokaa
upande msitunyanyase kwa kuwa uwezo wa kusimama na ninyi mahakamani hatuna tusaidieni
mtupe stahiki zetu kwenye mshahara mnatukata kutulipa hakuna ni unyanyasaji na udharirishaji
kwa watu wenye kipato kidogo