CWT WAZINDUA JENGO LAO MBEYA

Jengo la Chama cha waalimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Mbeya



CHAMA cha waalimu mkoani Mbeya kimezindua jengo lao kubwa jijini Mbeya lenye ulefu wa Ghorofa tano ambalo limejengwa na Suma-JKT kwa gharama ya fedha shilingi bilioni 1.4 za waalimu.
Jengo hilo limekabidhiwa na Suma – JKT kwa chama cha waalimu Mbeya mbele ya Rais wa Chama hicho taifa, Gration Mukoba na Meja Rafael Nguga mbele ya waalimu wa Mkoani Mbeya katika maeneo ya Sokomatola lilipo jengwa jingo hilo.
Akizungumza na waalimu wa Mbeya Rais wa CWT alisema kuwa jengo hilo ni la kwanza kwa ulefu kwa mkoa wa Mbeya na kwa Tanzania nzima kwa majengo ya waalimu.
Alisema kuwa Jengohilo litakuwa na ofisi ya mkoa, Jiji na Manspaa, na katika jingo hilo litakuwa na sehemu ya Benki yao.
Alisema kuwa jengo hilo ni miongoni mwa majengo 20 yanayo jengwa Nchi nzima ambayo mikoa mingime bado inaendelea kujengwa kwaajili ya ofisi za waalimu.
Rais wa Chama cha waalimtu Tanzania (CWT) Gration Mukoba
Aliongeza kuwa jengo hilo limejengwa kwa gharama wanazo katwa waalimu kila mwisho wa Mwezi na asilimia kubwa ya majengo wanayo jenga yamebakia kidoko kukamilika.
Mukoba alisema kuwa kulingana na pesa kidogo walizo nazo na mishahara midogo wanayo ipokea lakini wamefanikiwa kujenga majengo mazuri.
Alisema kuwa kulingana na pesa yao hiyo kidogo watafanya mambo makubwa na mazuri mambapo watajivunia kama waalimu.
Aidha alisema kuwa wazo la kujenga nyumba lilikuja baada ya kumuona konokono wa baharini na anakufa akiwa ameiacha.
Alisema kuwa nyuma hiyo imejengwa  kwa samani ya shilingi bilioni 1.4 ambazo zimekuwa zikikusanywa kidogokidogo kutoka kwa waalimu wenye mishahara midogo.