Kiasi ya watu 13 wameuwawa kufuatia shambulizi la kujitowa muhanga
lililofanywa na Taliban katika soko moja karibu na makao makuu ya jeshi la
Pakistan hii leo.
Ikiwa ni siku moja baada ya kushuhudiwa mashambulio
mabaya dhidi ya vikosi vya usalama ambapo wanajeshi 26 waliuwawa na kiasi
ya wengine 25 walijeruhiwa kaskazinimagharubu mwa mji wa Bannu.
Watu
wengine 18 wamejeruhiwa kufuatia mripuko uliotokea katika Rawalpindi mita
chache kutoka makao makuu ya jeshi.
Mashambulio hayo mawili yaliyotokea
ndani ya kipindi cha saa 24 yamedhihirisha kuongezeka kwa ghasia
zinazofanywa na kundi la Tehreel e Taliban TTP baada ya kipindi cha utulivu
kidogo kufuatia kuuwawa kwa kiongozi wake Hakimullah Mehsud aliyeuwawa
katika shambulio la ndege isiyokuwa na rubani lililofanywa na Marekani mwezi
Novemba.
Kwa mujibu wa taarifa ya afisa wa ngazi ya juu wa polisi Haroon
Joya waliouwawa kwenye mripuko wa leo ni pamoja na wanajeshi sita na raia
saba.
Dw.deSwahili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)