Jimbo la Upper Nile ladhibitiwa na jeshi la serikali

Jeshi la Sudan Kusini limesema hii leo kwamba limeuteka mji mkuu wa jimbo lenye utajiri mkubwa wa mafuta la Upper Nile ambako rais Salva Kiir alikuwa akitafuta  idhini ya bunge kutangaza hali ya hatari katika eneo hilo.
Mji wa Malakal ni njia inayotumiwa kwa ajili ya kufikia vinu vya mafuta upande wa kaskazini.Mapigano yameshuhudiwa kwa muda wa zaidi ya wiki moja kati ya jeshi na waasi katika eneo hilo.
Msemaji wa jeshi Kanali Phillip Aguer akizungumza na shirika la habari la dpa amesema kwamba vikosi vyake vimefanikiwa kuwatimuwa waasi kutoka mji huo wa Malakal mnamo majira ya mchana wa leo.
Aidha amesema waasi hawajulikani walikokimbilia lakini wameshatimuliwa ingawa hakutowa maelezo zaidi kuhusu watu waliojeruhiwa kufuatia mapigano makali yaliyotokea katika operesheni hiyo.
Rais Salva aKiir ametowa muda wa siku 15 bunge liidhinishe hatuwa ya kutangazwa hali ya hatari katika jimbo hilo la Upper Nile