WAOKOZI MBIONI KUFIKISHA MISAADA UFILIPINO

Wafanyakazi wa uokozi wako mbioni kuifikia miji ilioathirika na mawimbi kama ya tsunami ikiwa ni siku mbili baada ya kimbunga kikubwa sana cha Haiyan kupiga maeneo ya kati ya Ufilipino kikiwa na nguvu ya upepo uliokuwa ukisafiri kwa kasi ya kilomita 235 kwa saa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon
Kimbunga hicho hapo Ijumaa kilipiga visiwa sita vya Ufilipino vilioko katikati ya nchi hiyo na kusomba majengo na nyumba zilioko kwenye maeneo ya ufukweni.
 Kwa mujibu wa maafisa wa serikali takriban watu 10,000 inaaminika kuwa wameuwawa kutokana na kimbunga hicho ambacho kinatajwa kuwa mojawapo ya kimbunga kikali kabisa kushuhudiwa katika historia. 
Serikali inahofia idadi ya vifo inaweza kuongezeka.
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema mashirika ya misaada ya kibinaadamu ya Umoja wa Mataifa yanashirikiana na serikali ya Ufilipino kutowa msaada wa dharura kwa haraka.
Habari na DW.DE