Baadaye Obama atauongoza mkutano maalum wa Baraza la Usalama, linalotazamiwa kupitisha azimio juu ya kuzuwia wapiganaji wa kigeni kwenda Iraq na Syria. Kitisho cha kundi hilo la Dola la Kiislamu kilisababisha Marekani kufanya mashambulizi ya angani nchini Iraq mwezi uliopita, na jana ikatanua kampeni yake hiyo na kuzishambulia ngome zao nchini Syria.
Viongozi wa dunia kujadili kitisho cha IS
Viongozi wa dunia wanaokutana kwenye Hadhara Kuu ya
Umoja wa Mataifa, leo watazingatia kampeni inayoongozwa
na Marekani kuwaangamiza wapiganaji wa Dola la Kiislamu
nchini Iraq na Syria na hatua za kuwapiga marufuku
wapiganaji wa kigeni.
Rais Barrack Obama (Pichani) wa Marekani anayetafuta uungaji
mkono wa kimataifa dhidi ya wapiganaji hao, ni miongoni
mwa viongozi wa kwanza watakaohutubia katika mjadala
huo wa Baraza Kuu, unaoanza leo.