MGOMBEA wa chama cha
ACT-Wazalendo jimbo la Njombe kusini amekunana na somea zomea wakati akimnadi
mgombea Urais kupitia chama chache Anna Mgwila na kuonekana kumkandia mgombea
wa ubunge wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema baada ya kusema mgombea
huyo hataweza kuiondoa CCM.
Akizungumza katika kampeni zake katika kata ya Njombe mjini
mgombea wa Ubunge jimbo la Njombe kusini Emilian Msigwa alikutana na zomea
zomea baada ya kuanza kujinadi katika Ngome ya chama cha Chadema ambapo katika
jimbo hilo anakubalika na vijana ambao walikuwepo katika mkutano huo.
“Ndugu zangu wana Njombe nataka niwaambia kuwa katika
kipindi hiki wote tunataka mabadiuliko katika jumbo hili naombeni mnipekura
mimi na za Urais mumpe mama Anna Mgwila na udiwani mumpe diwani wa kata yenu
hasa wa Chadema kwa sababu sisi hatuma madiwani na nipo tayari kufanya kazi na
diwani yoyote,” alisema Msigwa na ndipo zomea ilipo anza.
Wananchi walio kuwepo katika mkutano howa walionekana
kukelwa na kusemwa kwa mgombea ubunge wa Chadema Emmanuel Masonga na kulkisikia
jina la Mgwila.
Msigwa akisema wamchague yeye na kuwa ataiondoa CCM
alikutana na sauti ya Ooooooh! Na akisema wamchague Mgwila zilisikika sauti za Rais
Lowassa bila mafanikoa na badayalake kuwaomba wananchi kuuliza mashwali kitu
kilicho ongeza zomeazomea kutokana na maswali aliyo kuwa akiulizwa na watu alio
dai kuwa wapo Chadema.
Kadri zomea zomea ilipo kuwa ikiongezeka vijana walizidi
kuongezeka ili kuona kinacho endelea katika mkutano huo, ambapo maswali yaliyo
kuwa yakiuliwa yalikuwa kakikazania kumchafua na kumfanya azidi kuzomewa.
Moja ya swali lililoulizwa katika mkutano huo ni pamoja na
kwanini anasema kuna wagombea anawaunga mkono wa Chadema alipokuwa Chadema lakini
aligombea nao mpaka alishindwa na kuhamia chama alichopo.
Akijibu swali hilo alisema kuwa wakati anagombea katika kura
za maoni za Chadema alisema kuwa ilionekana kuwa hata likiwekwa jiwe Chadema kinaweza
kushinda ndio maana na yeye aliingia kushindana licha ya kuwepo watu anao
wakubali.
Aidha Nestory Mkinga aliulizwa kuwa vyama vyote vya upinzani
lengo lake ni kukiondoa chama cha CCM lakini kwanini wanachama wa ACT
wasiungane Ukawa kuiondoa CCM.
Akijibu shwala hilo alisema kuwa vyama vyama vyote
vinakatiba yake na kuwa chama chake Katiba yake hairuhusu kujiunga na Ukawa.