ACT Wazalendo chaahidi kuweka nidhamu serikalini

Mgombea mwenza wa kiti cha Urais kupitia Chama cha ACT Wazalendo Hamad Yusufu amesema chama hicho kikiingia madarakani kazi ya kwanza itakuwa ni kuweka nidhamu serikalini ili kuhakikisha vitendo vya rushwa vinakwisha.

Ametoa kauli hiyo kwenye mkutano wake wa kampeni alioufanya mjini Babati mkoani Manyara.
Katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa kwaraa Babati, mgombea mwenza huyo wa urais kupitia ACT wazalendo amesema kwa kipindi cha miaka 50 chama cha Mapinduzi CCM hakijafanya lolote tofauti na kuendekeza rushwa iliyosabaisha umaskini.
Yusufu anasema kitu kingine kitakachopewa kipaumbele andapo chama hicho kitaingia madarakani ni kuboresha sekta ya elimu na kupitia mikataba yote ya wawekezaji.
Naye mgomea ubunge jimbo la Babati mjini kupitia ACT wazalando Biana Malya nasema kipaumbele chake ni kushughulikia afya.
Mgombea Mwenza wa chama cha ACT wazalendo Hamad Yusufu pia amewaombea kura wanaowania nafasi za udiwani kupitia chama hicho katika jimbo la Babati mjini.