KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema kama chama hicho kitashinda katika Uchaguzi Mkuu ujao, kitamaliza tatizo kubwa la maji lililopo mkoani Tabora.
Kabwe aliyasem,a hayo jana kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Mjini Tabora akiwataka wananchi kuhakikisha wanawachagua wagombea wa chama hicho kuanzia rais, wabunge na madiwani.
Alisema Ilani ya ACT, imeeleza wazi juu ya mpango wa chama hicho kuanzisha mfuko wa maji vijijini ambao utatumika kuendeleza, kulinda vyanzo vya maji na kukarabati miundombinu yake.
“Wakazi wa Tabora msiwe na wasi, jitokezeni kwa wingi kwenye vituovya kupigia kura mkaichague ACT ili tufanye kazi ya kuondoa kerokubwa ya maji,” alisema.
Aliwaomba wamchague Nicholaus Kayoka kuwa mbunge wa Jimbo la Ulyankulu, Amir Kirungi (Kaliua), Abraham Rupia (Sikonge), Kansa Mbaruku (Tabora Kaskazini) na Mapalala Kuziwa (Tabora Mjini).