Vikosi vya jeshi la Ufaransa limeshambuliana na waasi wa zamani katika jamhuri ya Afrika ya kati katika mji mkuu Bangui leo wakati wakijaribu kuwanyang'anya silaha wapiganaji baada ya ghasia ambamo mamia ya watu wameuwawa.
Jeshi la Ufaransa limeanza operesheni ya kuwanyang'anya silaha waasi , kwa nguvu ikiwezekana , hususan kundi ambalo linaundwa kwa kiasi kikubwa na Waislamu la Seleka na kundi hasimu la Wakristo.
Wanajeshi hao wameweka vizuwizi katika barabara kuu mjini Bangui na wanapekua kila gari wakitafuta silaha.
Mashambuliano ya silaha yalizuka karibu na uwanja wa ndege baada ya waasi wa Seleka kukataa kukabidhi silaha zao.
Msemaji wa jeshi la kimataifa la kulinda amani katika jamhuri ya Afrika ya kati FOMAC Celestin Christ Leon amesema kuwa waasi wa Seleka hawakutaka kunyang'anywa silaha na kukatokea mapambano ya silaha kwa muda. Mjini