KUHUSU MADELA: Ulinzi waimarishwa

Maelfu  ya  polisi  wa  Afrika  kusini  watawekwa  katika eneo  la  tukio  la  kumbukumbu  ya  Nelson Mandela katika  uwanja   wa  kandanda  wa  mjini  Soweto,  na maafisa  watazuwia  watu  kuingia  katika  eneo hilo iwapo watu  watakuwa  wengi  kupita kiasi. 
Waombolezaji  ikiwa ni pamoja  na  viongozi  zaidi  ya  70 kutoka  kote  duniani wanatarajiwa kumiminika  katika  uwanja  wa  Soccer City wenye  uwezo  wa  kuingia  watu  95,000. 
Mandela alijitokeza  mara  ya  mwisho  katika  uwanja  huo  siku  ya mwisho  ya  fainali  za  kombe  la  dunia  mwaka  2010. 
Luteni  kanali Solomon Makgale, msemaji  wa  jeshi  la polisi  nchini  Afrika  kusini  , amesema  kuwa  polisi  1,000 wataelekeza  magari, watawalinda  waombolezaji  na watasaidia  walinzi  wa  viongozi  ambao  watawasili  nchini humo  kwa  ajili  ya  tukio  hilo.
Miongoni  mwa  viongozi  wanaotarajiwa  kuwasili nchini Afrika  kusini  leo  na  kesho  ni  pamoja  na  rais Barack Obama  pamoja  na  mkewe Michelle Obama.
NA dw.de