Taifa
la Kenya sasa limejiunga katika orodha ya mataifa yenye pato la wastani
na kuondoka katika orodha ya mataifa yanayozingatiwa kuwa maskini baada
ya kufanyia mabadiliko mizani ya kukadiria ukuaji wa uchumi wake.
Mabadiliko
hayo yamehusisha upigaji upya wa hesabu ya thamani ya mapato
yanayotokana na mauzo ya bidhaa pamoja na huduma zinazotolewa na uchumi
wa taifa hilo - na pato la wastani limeongezeka kwa kiwango cha dola
bilioni 53 -ongezeko hili likiwa ni robo ya sehemu ya ukuaji wote wa
uchumi wa taifa hilo.Tathmini hii ya uchumi wa Kenya imeshuhudia bei ya bidhaa na huduma ikipanda huku pato la nchi pia ikipanda kwa mabilioni ya dola.
Takiwmu hizo mpya zinajumuisha sekta zinazoibuka ikiwemo teknolojia na sekta ya ujenzi na nyumba.
Kenya sasa iko katika nafasi ya nne huku uchumi wake ukiwa mkubwa zaidi katika kanda ya kusini mwa jangwa la Sahara kutoka katika nafasi ya sita. Imeipuki Ghana na Ethiopia.
Waziri wa mipango Anne Waiguru amesema kuwa data hiyo mpya inaonyesha kuwa uchumi wa Kenya ni mkubwa kuliko ilivyodhaniwa lakini hamanihsi kuwa viwango vya umaskini vimepungua wala kuongezeka kwa viwango vya utajiri.
Benki ya dunia inakadiria kuwa katia ya kila wakenya watano, wawili bado wanaishi katika umaskini mkubwa. Hata hivyo wadadisi wanasema ongezeko la pato la nchi litasaidia kupunguza madeni ya nchi na hivyo na hivyo ina maana kuwa nchi hiyo inaweza kukopa tena.
Hata hivyo, habari hii inaifanya nchi hiyo kuwa mahala pazuri wa kuekeza.