CHINA inaendelea kufanya makubwa kwenye ulimwengu wa teknalojia na sasa inazindua basi kubwa la aina yake ambalo kwa chini litaruhusu magari mengine kupita kama ilivyo kwenye daraja.
Mfumo huu mpya wa usafiri ni sawa na mwendo kasi zinazohudumia wakazi wa Jiji la Dar es Salaam lakini huu ni wa kisasa zaidi.
Basi hilo lenye mita mbili kwenda juu linaitwa TEB na litaanza kuhudumia umma wa Wachina kuanzia Agosti mwaka huu.
Likitumia nguvu ya umeme, basi hilo linauwezo wa kubeba hadi abiria 300 kwa mara moja huku likiwa na urefu wa futi 72 na upana wa futi 25. Basi hili litaweza kupita hata sehemu yenye foleni kwa sababu ya upana wake na nafasi ya wazi iliyo kwa chini ikiyaacha magari mengine kwenye foleni
Video ya basi hilo la kwanza kutengenezwa, ilizua mjadala huku likiwashangaza wengi baada ya kuwekwa hadhari mwishoni mwa Mei.
Majaribio ya basi hilo tayari yameshafanyika katika mji wa Qinhuangdao ulioko kaskazini mashariki mwa China.
Basi hilo ambalo lina uwazi mkubwa chini yake kiasi cha kuruhusu magari mengine kupita, linaweza kukimbia hadi kufikia kilomita 60 kwa saa huku likivuka reli pamoja na kupita katika njia za barabara za kawaida.
“Faida moja kubwa ni kuwa basi hili litatumia nafasi ndogo wakati linapokuwa ya barabarani,” Injinia wa mradi huo Song Youzhou aliliambia shirika la habari la China Xinhua.
Basi la TEB linafanya kazi kama ambavyo Subway linafanya lakini gharama za utengenezaji ni nafuu zaidi ukulinganisha na Subway,” anaeleza injinia mwingine Bai Zhimini.
Basi hilo la TEB litaweza kufanya kazi inayofanywa na mabasi ya kawaida 40 kulingana na maelezo ya watengenezaji wake. Hata hivyo, bado haijafahamika ni lini litatumika kwa wingi katika miji mbalimbali nchini China.
Kwa mara ya kwanza, wazo la kuwa na basi la aina hii lilionekana kama mzaha hasa baada ya kampuni inayolitengeneza kuonyesha mchongo mdogo kwenye maonyesho ya kimataifa ya teknolojia za hali ya juu ya Beijing.
Baada ya maonyesho hayo, kampuni mzalishaji ilitengeneza basi la kwanza ambalo lilifanyiwa majaribio na kuonyesha ufanisi mkubwa barabarani. Mamilioni ya watu walivutiwa na kushangazwa na basi hilo baada ya video yake kuwekwa mtandaoni.
Niliona picha za basi hili muda si mrefu uliopita lakini sasa naona zimegeuka kuwa basi kweli. Basi hili limejengwa kwa mwendo wa Kichina,” anasema mmoja wa watu waliolishuhudia basi hilo.
Likitazamwa kama mwarubaini wa foleni, TEB limeweza kuwa la aina yake kwa kuwa litaweza kutumia njia moja na magari mengine, pia halitalazimika kusimama wakati magari mengine yakisimama wakati wa foleni kali.
Barabara zetu bado zinakabiliwa na changamoto ya foleni,” anasema Wang Yimin mkazi wa mji ambao basi hilo lilifanyiwa majaribio ya kwanza.
Wazo la kutengeneza basi la aina hii lilikuwapo tangu mwaka 2010 wakati Jarida la Times lilipoandika makala ya kushawishi kampuni zenye uwezo kuwekeza kwenye usafiri ambao utasaidia kupunguza foleni barabarani.
Kampuni ya TEB Technology Development ilionekana kuvutiwa na wazo hilo na kuamua kulifanyia kazi. Mradi huo ambao kama utaweza kwenda kama unavyotarajia utasaidia tatizo la foleni na unaelezewa kuwa ni wa gharama nafuu ukilinganisha na aina nyingime za usafiri wa umma.
Vyombo vya habari vya Serikali ya China vilielezea kuwa uzinduzi wa huduma hiyo ulikuiwa wenye mafanikio makubwa huku tukio lake likivutia vyombo vya habari vya kimataifa kama shirika la habari la kimataifa la Reuters ambalo pia lilipewa nafasi ya kutembelea mradi huo pamoja na kufanya mahojiano ya kina.
Bila haka kama aina hii ya mabasi ingeletwa Tanzania na hususani Jiji la Dar es Salaam, pengine ingekuwa ni suluhisho la tatizo la kujazana kwenye mwendo kasi zetu ambazo zinaonekana kushindwa kuhudumia umma.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!
from Blogger http://ift.tt/2t8NIZb
via IFTTT