Madiwani wa CHADEMA washuhudia walivyohongwa hela na CCM ili wahame

Madiwani 6 wa Chadema wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha wamejiuzulu na kujiunga na CCM
Katibu wa Chadema kanda ya Kaskazini Amani Gulugwa amesema wana ushahidi wa CCM kuwahonga madiwani hao na wameshachukua hatua za kisheria kudhibiti mwenendo huo
Diwani wa kata ya Majengo Emmanuel Kivondo anasema viongozi wa CCM wanatafuta mbinu ya kukaa naye wazungumze lakini wanashindwa
CCM Arumeru nao wamekanusha vikali tuhuma hizo wakisema madiwani hao wamehama kwa hiyari yao wenyewe na bado wengine wapo njiani kujiunga na CCM kwani wanaona hawapo sehemu salama VIDEO:

from Blogger http://ift.tt/2tUZfyE
via IFTTT