Profesa Jay Afunguka Wema Sepetu Kuikacha Harusi yake

BAADA ya Jumamosi iliyopita Mbunge wa Mikumi kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Haule ‘Profesa Jay’ kufunga ndoa na mchumba’ke wa kitambo, Grace Mgonjo katika Kanisa la Mtakatifu Joseph lililopo Posta jijini Dar na sherehe kufanyika ndani ya Ukumbi wa Mlimani City, ameibuka na kufunguka suala la Miss Tanzania 2006/07, Wema Sepetu kuikacha harusi yake.
Taarifa za awali kutoka kwa chanzo makini zilieleza kuwa, Profesa Jay na Wema ambaye alihamia Chadema miezi kadhaa iliyopita wana bifu kali japokuwa haijulikani chanzo ni nini, ndiyo maana mwanadada huyo hakuhudhuria kwenye harusi hiyo.
“Unajua Wema na Jay hawana uhusiano mzuri tangu ahamie kwenye chama hicho yaani wana bifu ndiyo sababu hata Wema hakuhudhuria kwenye sherehe ya harusi ya Jay maana wangekuwa sawa ungeona mbwembwe zake ukumbini lakini hakutokea,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, Risasi Jumamosi lilimtafuta Profesa Jay kwa njia ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp akiwa honeymoon ambapo mahojiano yalikuwa hivi;
Risasi Jumamosi: Hongera kwa kuoa na kuachana na ubachela Jay. Profesa
Jay: Asante sana, karibu.
Risasi Jumamosi: Kuna habari kuwa wewe na Wema mna bifu ndiyo maana hakuhudhuria hata kwenye harusi yako, hili likoje?
Profesa Jay: Jamani watu hawaishiwi maneno! Wema ni kamanda wangu tena tunahesh
imiana kwelikweli nisizuliwe bifu zisizokuwa na kichwa wala miguu.
Risasi Jumamosi: Kwa nini sasa hakuwepo au hukumwalika?
Profesa Jay: Mbona kuna watu wengi tu hawakuhudhuria kwa nini Wema? Mwacheni dada yangu apumzike, acha hizo stori. Profesa Jay kwa upande mwingine alieleza kuwa kesho Jumapili anatarajia kufanya sherehe kubwa kuliko ya mwanzo huko jimboni kwake Mikumi ambayo kila mwananchi atahudhuria kwani hakutakuwa na kadi na itafanyika uwanjani ikiwa ni shukrani kwao kwa kumchagua kuwatumikia

from Blogger http://ift.tt/2te6N0v
via IFTTT