KATIBU Mkuu wizara ya Maliasili na Utalii Dkt Adelhelm Meru
imethibitisha kuanza kuwalipa fidia wakazi wa vijiji kadhaa wilayani
Mbarali mkoani Mbeya, ambao wamepunjwa fidia zao na wengine
hawakulipwa kabisa.
Ametoa kauli hiyo mkoani Mbeya jana wakati wa uzinduzi wa mradi mkubwa
wa uendelezaji wa sekta ya utalii ukanda wa kusini unaofadhiliwa na
Benki ya dunia kwa gharama ya shilingi Bilioni 200.
“Tayari nimetoa agizo kwa Mamlaka ya Hifadhi nchini-Tanapa ili
kuhakikisha wanafanya uchunguzi na kubaini wananchi wa Vijiji hivyo
ambao hawajalipwa, lakini pia kuwabaini wananchi ambao wamepunjwa
malipo, kuanza mara moja kuwalipa, Dkt Meru alisema.
“Wananchi hao ambao mara kadhaa wamekuwa wakiandamana hadi ofisi za
Mkuu wa wilaya ya Mbarali kudai fidia hizo, bila mafanikio, kwa sasa
tatizo hilo litabaki kuwa historia.
Licha ya kwamba Dkt Meru hakutaka kubainisha kiasi cha fidia
kinachodaiwa na wananchi hao lakini amethibitisha kuwa Tanapa
watawalipa wananchi hao.
Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Mbeya akiwa mwenyeji wa wakuu wa mikoa
watakao nufaika na mradi huo Abbas Kandoro alisema mradi huo ni
uendeleza na kukuza sekta ya utalii ukanda wa kusini.
Kandoro amesema mradi huo utafungua fursa ya ajira kwa wananchi wa
mikoa hiyo, lakini pia utaboresha miundombinu mbalimbali iwe rafikii
kwa watalii wa ndani na nje ya Nchi.
“Kwa mfano utajenga barabara zinazoingia kwenye vivutio vya utalii,
ujenzi wa madaraja na utakarabati fukwe ambazo ziko katika mikoa ya
kusini,” alisema Kandoro.
“Aidha mradi huo utaongeza fursa nyingi za utalii kwenye mikoa hiyo ya
kusini ili ifanane na fursa iliyopo Kanda ya kaskazini, mara kadhaa
kanda ya kusini ndio inayoongoza kuwa na vivutio vingi vya utalii,”
aliongeza kueleza Kandoro.
Hata hivyo kamati ya wahanga wilayani humo inayo ongozwa na mwenyekiti
wao Patiliki Myota amesema Tanapa inatakiwa kulipa fidia hizo haraka
kwa wananchi wahanga wa vijiji hivyo vilivyo pisha mradi huo.
Myota alisema mradi huo uligusa kata nne Msangaji, Mawindi,Utengule na
kata ya Madibula ambapo kata ya Masngaji ikijumuisha vijiji vyote na
kata ya Mapogoro kijiji cha Isimikwe, wakati kata ya Mawindi kuna
vijiji vya Tagawanu, Kapunga na Ukwava.
Alisema kata nyingine ni Madibira ambayo vijiji na vitongoji vilivyo
pisha ni Ikoga na Utengule ambapo kwa julma ya wakazi walio hama
kupisha mradi huo ni 6009 ambapo matarajio makubwa kwa wananchi hao ni
kuweza kulipwa fidia zao haraka.
Mwenyekiti huyo alisema hadi sasa ni miaka nane imepita huku wananchi
hao wakiwa na matumaini ya kulipwa ikiwa ni pamoja na ahadi kutoka kwa
viongozi mbalimbali waliofika bila kupatiwa haki yao.