Vijana na Mapadre waonywa kuingia katika makundi ya watangaza nia


ASKOFU wa jimbo kuu la Songea Damian Dallu amewataka mapare nchini kote kuto jiweka katika makundi ya watangazania ambao wanaendelea kutangaza nia hapa nchini ili kuto kuwapo kwa mgawanyiko wa makundi na kusababisha mpasuko wa kitaifa.

Kauli hiyo imetolewa wakati wa misa ya kufunga kongamano la vijana kitaifa lililofanyika Mkoani Njombe ambapo amewataka mapadre na vijana kutokujiingiza katika makundi ya watangaza nia ambao wanaendelea kutangaza nia hapa nchini.

Alisema kuwa endapo mapadre watajikita kwa makundi kwa mtangazania mmoja mmoja wata sababisha mpasuko atakapo teuliwa mmoja kugombea urais.

Askofu Dallu alisema kuwa pamoja na mapadre kuto kuwa na vyama alisema kuwa vijana nao wahakikishe wanaimalisha utaifa na sio kujikuta katika umoja wa vijana wa vyama vya siasa.

Alisema kuwa vyama vya siasa vipopo na wakiingia katika vyama hivyo wanaweza kuanza kupingana wao wenyewe cha msini ni kuungana katika umoja wa vijana wa taifa na sio wa vyama vya siasa.

“Vijana angalieni kuto kujikuta katika umoja wa vijana wa vyama vya siasa jiungeni na unganisheni taifa katika umoja wa vijana wa taifa na sio kujikita katika vyama vya sisasa,” Alisema Dallu.

Alisema kuwa Wakrel (Mabruda) wajishirikishe na siasa kwa asilimia ndogo sana na sio kujihusisha na siasa hadi kufikia hatua ya kuwa na watu wengi.

Aidha aliwataka vijana kuto jiingiza katika siasa ambayo inaweza kusababisha mgawanyiko wa taifa ambalo limetufikisha hapa.

Alisema vijana wawemakini na vijana na wanasiasa wanao taka kulivunja taifa na kuachana nao na kutoa taarifa kwa vyombo vinavyo husika ili kuepusha taifa kuingizwa katika machafuko.