KANISA LA KISASA KUJENGWA MAKOLE DODOMA NI LA PENTECOSTAL HOLINESS

Kazi ya Ujenzi wa Kanisa jipya la Pentecostal Holiness Association mission Makole Dodoma inaendelea kwa awamu nyingine hatua tulio nayo sasa tumemwaga zege kwenye msingi kati ya nguzo na nguzo kazi hiyo imefanyika jana na wiki hii tutaanza kujenga tofali za msingi tunatakiwa kuwa na tofali zisizopungua 4500 lakini mpaka sasa tunazo tofali 1900 na mifuko ya cement inaitajika 30 mpaka sasa tunayo mifuko 10. Tuungane pamoja wenzetu mlio mbali nje ya Dodoma, Nje ya Tanzania, Nje ya Africa. Tujenge pamoja nyumba ya kuabudia. Mwampona Katibu wa Ujenzi.