WADAU wa mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi Mkoani Njombe wameishauri serikali kugawa lishe kwa watu wanapo enda kupada dawa za kupunguza makali ya VVU badala ya kugawa kinga za ugonywa huo na kuwa kwa kugawa kinga hizo wanawashawishi wakafanye uzinzi.
Wakizungumza katika mkutano wa wadau wa mapambano dhidi ya Ukimwi walisema kuwa ni bora wakati wa kuchukua dawa wakawa wanapata chakula kwaajili ya kwenda kuimarisha afya zao wakati wanakunywa dawa hizo kuliko kupewa Kondom.
Mmoja wa wadau aliyezungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza mkutano huo Grace Kambindu alisema kuwa ni bora wakati wa kuchukua dawa kukawa kuna tolewa unga wa lishe ili kuimarisha afya za wananchi waishino na maambukuzi.
Alisema wanapo toa kondom wanawahamasisha kwena kufanya na kupoteza nguvu kuliko wange wapa chakula.
“Serikali huko inakoomba msaada ni bora ikaomba msaada wa unga wa lishe ambao utakuwa ukutolewa kwa wanao enda kuchukua dawa za kupunguza makali ya VVU, ARV’s kuliko kutoa kondom kwa sababu mtu akifanya ngono humaliza nguvu, kikitolewa kikombe kimoja watasaidia zaidi kuliko kutoa kondomo,” alisema Grace.
Akizungumzia alivyo ushinda ufanyaji wa ngono baada ya kufariki mumewe mjane huyo amesema kuwa hajawahi kufikilia kuolewa na kuwa amejikita katika shughuli zake za kila siku na kufanya familia yake kuendeleza na maisha ya kawaida.
Alisema wananchi wakijikika katika ufanyaji kazi na kujiweka bize hawata fikilia kufanya ngono na watapuguza uwezekano wa kupata ugonjwa huo ambao unatishia maisha ya Watanzania na nguvu kazi ya taifa.
Aidha mratibu wa Mwakilishi wa mratibu wa Ukimwi Mkoani Njombe Dr. Godfrey Baragona alisema kuwa wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kujua idadi ya wanaowapatia dawa hizo kutokan ana wengine kuacha matumizi ya dawa bila kutoa taarifa ama wengine kuhama vituo na kusababisha kuto jua waliofariki.
“Tuna vituo vya utoaji huduma endelevu CTC 40 na watu walio jiandikisha katika votuo hivyo awali ni zaidi ya wagonjwa 57,000 na asilimia 53 ndio wanaendelea kuja kupata huduma walio baki hawaeleweki kama wapo ama wamehama vituo au wameacha kutumia dawa kwa kuwa hakuna taarifa tulizo nazo, alisema Dr. Baragona.
Kutokana na hali hiyo alitoa ushauri kwa wananchi kama ndugu amefariki kutoa taarifa ili serikali kujua walio fariki na kuweka kumbukumbu zake vizuri, na kuongeza kuwa serikali inaumuhimu wa taarifa hiyo kuliko mwananchi anavyo fikiri.