Claudio Bravo aipeleka Chile fainali, Ureno chali

Hakika ulikuwa mchezo mgumu sana kama ulivyotarajiwa kati ya mabingwa wa Ulaya timu ya taifa ya Ureno dhidi ya Chile ambao ni mabingwa wa America.
Mchezo huo wa nusu fainali ya confedaration cup ulimalizika dakika 90 kukiwa hakuna timu iliyopata bao na hata zilipoongezwa 30 ili kumalizia 120 milango bado ilikuwa ni migumu.
Baada ya hapo muamuzi aliamuru kupigwe mikwaju ya penati ambapo ndio Ureno waliondolewa baada ya Chile kufunga mikwaju yote mitatu ya mwanzo ya penati huku Wareno wakikosa.
Shukrani kwa mlinda lango wa Chile Claudio Bravo ambaye aliokoa penati tatu za Ricardo Quaresma, Moutinho na Nanj huku za Chile zikiwekwa kambani na Vidal,Sanchez na Aranguiz.
Baada ya mchezo huo ambao Bravo anyeidaki Man City alikuwa mchezaji bora wa mechi sasa Chile wanakwenda fainali wakisubiri mshindi kati ya Ujerumani na Mexico kwa ajili ya fainali hiyo ya Confedaration Cup.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2skhluH
via IFTTT