- CHELEWENI KUNUNUA HUENDA BEI IKASHUKA
- HATAZIKIWEPO MASHINE MAKANJANJA WA TRA WATAKUWEPO TU
- KINANA NI KAMA MWALIMU JK
WANANCHI wametakiwa kuendelea kubisha kununua mashine za
kielekroniki za kutolea risiti (EFD) ili zizidi kushuka bei.
Hayo yalibainishw ana Kinana wqakati akizungumza na wananchi
wa Mkoa wa Mbeya katika mkotano wa Hadhara ambapo alisema kuwa waendelee kusita
kununua mashine hizo ili kusababisha ziendelee kushuka bei.
Alisema, kuwa mashine hizo awali zilikuwa zinauzwa kwa bei
ya shilingi milioni 2 na zikashishwa mpaka milioni 1.2 na sasa zinauzwa kwa shilingi
laki 8 ambapo wakiendelea kusitakununua huenda zikashuka zaidi.
Alisema, yeye ana hoji ni kwanini zinashuka bei na je
zinatofautigali na aliye nunua wakati ule zilikuwa zinanini na sasa hazina nini
mpaka zikashuka bei kiasi hicho.
“Je wananchi wange nunua kwa wakati ule zinauzwa milioni 2
maana yake pesa za hapo juu kutoka milioni 2 hadi laki 8 zingeliw ana wajanja
kunanini kunaupunguzwaji wa bei kama hazinautofauti au kuna wajanja wana kula
cha juu,” alisema Kinana.
Alisema, kuwa mashine
hizi zimeletwa ikiwa ni mara ya tatu ambapo mashine za kwanza kuletwa ziliondolewa
na kuwa hazifai zikaletwa zingine nazo zikaondolewa na sasa zimeletwa hizi
wananchi wataziamini vipi kama zinafaa na haziko kama zile za awali zilizo
ondolewa.
Kinana alisema, mashine hizo inadaiwa kuwa zitakuwa
zikizibiti ulipaji wa kodi na kuwabana walio kuwa wakipitia njia za panya na
kujinufaisha lakini yeye hana imani kwa asilimia zote kama mashine hizo
zitaweza kudhibiti wala rushwa badara yake watabuni njia za kuchukua rushwa
hata kama kuna mashine hizo.
“Mashine hizi hazita zuia moja kwa moja walarushwa wanao
kula rushwa badala yake watabuni njia nyingine ya kuchukua rushwa kwa
wafanyabiashara hata zikiwepo mashine hizo,” alisema Kinana.
Alisema maelezo yaliyo tolewa kuhusiana na mashine hizo ni
mazuri sana sasa kama serikali inataka mwananchi huyo alipekodi vizuri ingetoa
mashine hizo ili kuhakikisha analipa kodi vile inavyo takiwa.
“Kama serikali inataka kukusanya kodi inezitoa mashine hizo
kwa wafanyabiashara bure kwa wafanyabiashara wanao anza biashara na kuangalia
makusanyo ya kodi bara baada ya kuona biashara inaenda vizuri ataendelea
kuitumia na kama haitaenda vizuri anyang’anye kuliko inavyo fanya hivi sasa na
kudai itarudisha kidogokidogo kwa mwananchi pesa alizonunulia,” Aliongeza Kinana.
Kinana alisema kuwa serikama inampango wa kurudisha pesa
hizo kwa mfanyabiashara anayetumia mashine hizo ingependeza kama mashine hizo
zingetolewa bule kwa wafanyabiashara kama mkopo ili wawakape katika kodi
wanayoikusanya.
Hivyo aliwataka wafanyabiashara hao kuchelewa kununua
mashine hizo ili kusubili bei zishuke kama zilivyo shuka kutoka milioni 2 hadi
laki 8 hivi sasa.
Mashine hizo zilisababisha wafanyabiashara kufunga maduka
yao wakizikataa mashine hizo na kusababisha polisi kutupa mabomu na kumwaka
maji ya kuwasha kwa wafanyabiashara wa Mbeya na wafanyabiashara wa Soko la
Kaliakoo jijini Dar es salaam nao wakizipinga mashine hizo kugoma kufungua
maduka yao.
Kufuatia kusitasita kuzitumia mashine hizo za EFD serikali
iliongeza muda wa kufikia ukomo wa kutumia vitabu vua risiti madukani na
kutumia mashine kutoa lisiti na kuwa mwisho wake kuwa ni disema 31 ili kusubili
ambao hawajanunua wanunue.
Kinana alisema nda huo ulio ongezwa hautoshi hivyo iongeze
mda wa ukomo wa utumiaji wa vitabu katia utoaji wa risiti.