KATIBU mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abrahaman Kinana ameitaka
serikali kurudisha viwanda vyote vilivyo kufa iuli kuongeza ajira kwa vijana.
Akizungumza na wakazi wa jiji la Mbeya katika Mkutano wa
hadhara uliofanyika katika viwanya vya Ruanda Nzovwe jijini humu, Kinana
alisema kuwa serikali ivirudishe viwanda vyote ili kuleta ajira kwa vijana
ambao wapo mtaani na kukosa ajila.
Kinana alisema, kuwa Mkoa wa Mbeya zamani ulikuwa na viwanda
vingi lakini vilibinafsishwa na viongozi wa serikali nia na kuzitafuna pesa na
waliovichukua kushindwa kuviendeleza kisha kufungwa.
Alisema kuwa mtu alipo kuwa anataka kuchukua kiwanda alisema
atakiendeleza lakini imekuwa kintume nma viwanda vingi vimekufa na kusababisha
nchi kuw ana vijana wengi wasio kuwa na ajila.
“Viwanda vingi vilipo kuwa vikibinafsishwa ilidaiwa kuwa
vitaendeleza chaajabu waliokuwa wakivichukua walishindwa kuviendeleza na
hatimaye kuvifanya kuwa maghala ya kuhifadhia vitu mbalimbali,” Alisema Kinana.
Aidha kinana alisema kuwa atakutana na watu wanao husika na
viwanda serikalini na kufanya utaratibu wa kuvirudisha viwanda hivyo ili kuleta
ajira kwa vijana wa kitanzania ambao wengi wapo mtaani pasipo kuwa na ajira
yeyote.
Alisema kuwa walioshidwa kuviendesha viwanda hivyo
wavirudishe serikjalini ili viendelezwe na kuzalisha ajira kwa wananchi na kuwa
anajua kuwa viwanda hivyo avitarudishwa hivihivi na vitauzwa.
“Viwanda hivyo havitarudishwa bure najua vitauzwa na katika
uuzaji huo kunawatu watapata ulaji na hakunakukwepa wajanja wengi hapa nchini,”
aliongeza Kinana.
Kinana
alisema kuwa serikali ichukue mashamba ambayo muwekezaji ameshindwa
kuyaendeleza ambayo kwa sasa yamekuwa yakikodishwa kwa wananchi.
“Serikali iyachukue mashamba ya Mpunga ambayo yalibinafsishw
ana serikali kwa lengo la kuongeza ajira kwa wananchi ambapo muwekezaji alisema
kuwa atayasimamia na kuleta ajila sasa anakodisha kwa wananchi kinyume na
alivyo takiwa kufanya alivyo sema wakati anachukua,” Alisema Kinana.
Katika mkutano huo ambao ulihudhuliw ana wananchi kutoka
katika kona mbalimbali za wananchi walio fika katika mkutano huo walisema kuwa Kinana
ni kama Hatati Baba wa Taifa Julius Nyerere kwani vitu alivyo visema vipo
tofauti na viongozi wengine wa CCM.
Walisema kuwa kuhusiana na ufufuaji wa viwanda atatusaidia
kuboresha maisha yetu na kupata ajira kitu ambacho hakijawahizungumzwa na
viongozi wengene wote.
Mmoja wananchi walio
kuwapo katika mkutano huo wa adhara, John Mkombe, akizungunza na Elimtaa
kuhusiana na kile kilicho zungumza na Kinana alisema, kuwa maneno analiyo
yasema Kiongozi huyo ni kama Mwalimu (Baba wa Taifa) kwani amezungumza vitu
vinavyo wagusa moja kwamoja.
Alisema viongozi wengine wakekuwa wakija na kutaka wapigiwe
makofi na kuzungumza vitu ambavyo havina tija kwao na kuonge kwa kuilinda
serikali lakini Kinana ametoa maneno makali kwa serikali.
Kinana alisema kuwa atazungumza na Rais Jakaya Kikwete
kuhusina na ufufuaji wa viwanda ili viwanda vifuifuliwe na wananchi wapate
manufaa ya viuwanda hivyo