HISTORIA FUPI YA HAYATI NELSON MANDELA 'MADIBA'

Nelson Rolihlahla Mandela ni Rais wa kwanza Mwafrika wa Afrika Kusini ya kidemokrasia. 
Ni mtu aliyejijengea heshima kubwa duniani kutokana na jitihada zake kubwa zilizofanikisha uhuru wa nchi hiyo na nyinginezo katika Bara la Afrika.
Hatati Mandela anayefahamika pia kwa jina la Mzee Madiba amelazwa hospitalini mjini Pretoria, Afrika Kusini kwa zaidi ya mwezi sasa akiwa mahututi. Anasumbuliwa na ugonjwa wa mapafu.

Kutokana na umaarufu wa Rais huyo mstaafu wa Afrika Kusini mwenye aliyefariki akiwa na umri wa miaka 95, Elimtaa tumeona vema kuchapisha historia fupi ya maisha yake kama ifuatavyo:

Nelson Mandela ni mwanasiasa mkongwe na mwanaharakati aliyepambana na sera za ubaguzi za makaburu wa Afrika Kusini na hatimaye kuwa Rais wa kwanza Mwafrika nchini humo. Ni mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel. Pia amepata kutunukiwa zaidi ya tuzo 250 katika miongo minne iliyopita.

Ni rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia nchini Afrika Kusini. Alikuwa mwanasheria na mwanachama wa Chama cha African National Congress (ANC) aliyepinga utawala wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini.

Nelson Mandela alizaliwa Julai 18, 1918. Baba yake mzazi alifariki wakati Mandela akiwa na umri wa miaka tisa. Tangu kipindi hicho alilelewa na Jonintaba hadi alipoitoroka familia hiyo baada ya kutakiwa aoe mwanamke aliyepangiwa.

Mwaka 1943 Mandela alijiunga ANC. Aliiongoza Afrika ya Kusini dhidi ya ubaguzi wa rangi na kuibuka kiongozi shujaa duniani.

Alipoanza mapambano ya kupinga utawala wa ubaguzi wa rangi na kutafuta usawa kwa wote, ilitegemewa kuwa mke wake ndiye angekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha mambo yanakwenda sawa.

Mandela alipata kuoa wake watatu katika historia ya maisha yake. Alimuoa mke wa mwisho siku alipokuwa akiadhimisha miaka 80 ya kuzaliwa kwake.

Madiba anatajwa kuwa katika kipindi chote cha historia yake amekuwa akiwaunga mkono watoto na upatikanaji wa elimu. Mfuko wa Nelson Mandela wa kusaidia watoto ni sehemu tu ya ushahidi wa mafanikio ya Mandela kuwasaidia watoto.

Mandela ni baba wa watoto sita. Watoto wanne aliwazaa na mke wake wa kwanza, Evelyn Mase na watoto wawili aliwazaa na mke wake wa pili, Winnie Madikizela.

Inaelezwa kuwa baadhi ya watoto wake hawakupata kwenda kumwona Madela alipokuwa gerezani.

Watoto wake wote wawili wa kike aliowazaa na mke wa kwanza walikuwa wakitumia jina la Makazawie.

Mtoto wake wa kwanza alifariki akiwa na umri wa miezi tisa na mtoto wa pili aliyejulikana kwa jina la Madiba Thembikile (Thembi) alifariki katika ajali ya gari mwaka 1969 akiwa na umri wa miaka 25. Mandela alikuwa gerezani na hakuruhusiwa kwenda kuhudhuria mazishi ya mwanaye.

Mtoto mwingine, Makgatho alifariki kwa ugonjwa wa Ukimwi mwaka 2005. Mandela amekuwa mstari wa mbele kupiga vita virus vya Ukimwi na Ukimwi akitumia namba 46664 ambayo ni namba yake alipokuwa gerezani kupiga kampeni.

Mandela na Evelyn walidumu katika ndoa yao kwa miaka 13 kabla haijavunjika mwaka 1957. Evelyn alikuwa muumini wa dhehebu la Mashahidi wa Yehova lililokuwa haliruhusu waumini wake kushiriki kwenye siasa, hivyo muda wote hakujihusisha na siasa. Alifariki mwaka 2004.

Mandela alimuoa Winnie Madikizela mwaka 1958, ingawa muda mwingi hawakuishi pamoja kwa sababu alikuwa kifungoni huku Winnie akijijengea umaarufu katika majukwaa ya siasa.

Kutokana na misuguano iliyoibuka ndani ya umaarufu wa kisiasa ya Mandela na Winnie walijikuta wakipeana talaka mwaka 1994. Mwaka 1998 Mandela alimuoa Graca Machel ambaye alikuwa mke wa kwanza wa Rais wa Msumbiji, Samora Machel.

Rais wa sasa wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, ameendelea kutoa wito kwa wananchi wa nchi hiyo wamwombee heri wakati huu anapougua. Maombi yamekuwa yakifanywa makanisani kote nchini Afrika Kusini kumwombea Mandela apone maradhi yanayomsumbua.

Hata hivyo, Mandela kabla ya kufa alikuwa ameshaandika wosia wake na kuelekeza kwamba kama atakufa azikwe kwenye milima iliyojitenga nyumbani kwa mababu zake huko Qunu, Afrika Kusini.

Mandela alikuwa Rais wa Afrika Kusini kuanzia mwaka 1994 hadi 1999. Alifungwa jela miaka 27 kuanzia mwaka 1962 hadi mwaka 1990. Anaelezwa kuwa alikumbwa na ugonjwa wa mapafu alipokuwa akifanyishwa kazi ngumu katika machimbo ya mawe akiwa gerezani.