HAYA NDIYO ALIYO YAFANYA ENZI ZA UHAI WAKE
Kwa wale waliofuatilia maisha yake kwa karibu, Nelson Mandela alikua kama mtu aliyezaliwa kuwa kiongozi.
Kama rafiki yake waliyefungwa naye pamoja,Ahmed
Kathrada, alivyosema hivi karibuni, Mandela alizaliwa katika familia ya
kifalme na ilikuwa kaiwada kwake kua alizaliwa kua kiongozi.Ingawa Mandela alijitaja mwenyewe kuwa kama sehemu tu ya uongozi wa ANC, hapakuwa na shaka kuwa alikuwa kiongozi mkuu wa chama hicho kwa kizazi chake wakati huo nchini Afrika Kusini.
Hakuwa na machungu na De Klerk
Kwa dunia nzima Mandela alikua ishara ya mambo mengi, sio kiongozi tu lakini mfano wa viongozi ambao dunia insatahili kua nao enzi hizo.Wengi wanamfahamu Mandela kwa kua na moyo mwepesi wa kusamehe na wengi wanamkumbuka hivyo kwani baadhi walimshangaa sana miaka ya tisini, aliposema kuwa hana chuki na mtu na kuwa amewasamehe waliomtendea ubaya na hata kumfunga. Hakuwa na uchungu wowote na FW De Klerk.
Msimamo wake ulijulikana na kufafanuliwa vyema katika kesi iliyohujumiwa mwaka 1964. Alisema, ‘Nimepigana dhidi ya ubaguzi wa rangi na pia nimepigana dhidi ya utawala wa waaafrika weusi usiofaa.’’
"Nimekuwa nikiota kuhusu jamii huru, ambapo kila mtu ataishi na jirani yake bila uhasama, wala chuki na kuwa na fursa nzuri. Lakini pia ikiwa itahitajika, ninaweza kutoa uhai wangu kwa ajili ya vita kama hivi."
Alizaliwa mwaka 1918,katika Rolihlahla Dalibhunga, na kulelewa katika kijiji cha Mvezo Mashariki mwa mkoa wa Cape. Alikuwa na ndugu zake 13 katika familia iliyokuwa na uhusiano wa karibu na familia ya kifalme ya Thembu.
Lakini alimsifu sana babake kwa kumsisitizia kuwa na maadili mema kwani yeye ndiye alimfanya kua mtu mwema maishani.
Miaka mingi baadaye Mandela alisema kuwa babake alikuwa mtu mtukutu ila alifanya hivyo kwa misingi ya usawa, kutaka kila mtu aishi bila kudhulumiwa, alisema babake alibadili maisha ya kijana mdogo mwenye ndoto kubwa.
Mandela aliishi kijijini ambako alifunzwa namna ya kua kiongozi.
Ilikua muhimu kwake kupata elimu. Na hivyo akasomea katika shule ya kimethodisti, na kisha mwaka 1939 akaenda katika chuo kikuu cha Fort Hare .
1918 Alizaliwa katika mkoa wa Eastern Cape
1943 Akajiunga na chama cha ANC
1956 Alifunguliwa kesi ya uhaini lakini baada ya miaka mine kiasi ikatupiliwa mbali
1962 Alikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la uchochezi na kufungwa jela miaka mitano
1964 Alishitakiwa kwa kosa la kuhujumu serikali na kufungwa maisha jela
1990 Aliachiliwa kutoka gerezani
1993 Ashinda tuzo ya Amani ya Nobel
1994 Alichaguliwa Rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini
1999 Ang’atuka mamlakani
2001 Aligunduliwa kua na Saratani ya tezi kibofu
2004 Alistaafu
2005 Alitangaza kua mwanawe alifariki kutokana na maradhi ya
1943 Akajiunga na chama cha ANC
1956 Alifunguliwa kesi ya uhaini lakini baada ya miaka mine kiasi ikatupiliwa mbali
1962 Alikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la uchochezi na kufungwa jela miaka mitano
1964 Alishitakiwa kwa kosa la kuhujumu serikali na kufungwa maisha jela
1990 Aliachiliwa kutoka gerezani
1993 Ashinda tuzo ya Amani ya Nobel
1994 Alichaguliwa Rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini
1999 Ang’atuka mamlakani
2001 Aligunduliwa kua na Saratani ya tezi kibofu
2004 Alistaafu
2005 Alitangaza kua mwanawe alifariki kutokana na maradhi ya
Wote wawili walifukuzwa kutoka chuoni kwa sababu za kisiasa
Mwanzo alikua wakili kisha mwanaharakati na kisha akaanza vita dhidi ya utawala wa wazungu.
Miaka ya hamsini na mapema miaka ya tisini, wakati maandamano yao yalipotibuliwa kwa nguvu, chama cha ANC kikaanza vita haslisi dhidi ya utawala wa wazungu.
Alikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la uhaini mwaka 1956.
Baada ya kesi yake kudumu miaka mitano, aliachiliwa huru.
Lakini ANC kikawa kimepigwa marufuku naye Oliver Tambo akatoroka nchi hiyo.
Mandela naye pia alijificha na kuendeleza harakati zake kichinichini na kuanza safari zake nje ya nchi kutaka usaidizi kwa mataifa mengine. Pia alimtembelea Tambo mjini London.
Lakini aliporejea ndiposa akakamatwa na kufungwa maisha jela, kwa miaka 27 kwa madai ya kuhujumu serikali.
Alifanya kazi katika machimbo ya mawe akiwa gerezani katika kisiwa cha Roben. Daima alisema gerezani alikua na muda mwingi wa kutafakari maisha.
Baada ya kuondoka jela mwishoni mwa kifungo chake cha miaka 27, maisha ya Mandela yalikuwa yamekomaa, na ilikua dhahiri kua walimnyang’anya Mandela ujana wake.
Ndoa yake kwa Winnie Mandela ilimalizika baada ya wawili hao kuachana. Marafiki zake wakawa hawapo tena.
Lakini alipokewa vyema sana na umati mkubwa wa watu alipoondoka gerezani.
Katika hali hiyo, angekuwa kiongozi mwingine, angemlaumu adui wake lakini Mandela pia aliwalaumu waafrika wenzake hasa wa chama cha ANC aliosema wanawaua watu na kua waache tabia hiyo.
Alijua watu wasingependa ujumbe wake, lakini pia alijua hawatamsikiliza.
Chama cha ANC kilishinda kwani watu wengi walikuwa na imani nacho.
Na BBCSWAHILI