WANACHAMA wa
chama cha Madibira Saccos Wilayani Mbarali
mkoa wa Mbeya wameutaka uongozi wa chama hicho kuhakikisha unakusanya
madeni kutoka kwa baadhi ya wanachama ambao wameshindwa kurejesha fedha za
mikopo mbalimbali kwa wakati.
Kauli hiyo
imetolewa na wanachama hao jana kwa nyakati tofauti ,katika mkutano mkuu wa
kawaida wa 13 wa chama hicho uliofanyika katika Ukumbi wa shule ya Sekondari
Madibira.
Walisema
kuwa mbali na kuwepo kwa baadhi ya wanachama ambao wamekuwa na madeni
sugu,lakini kumekuwepo na hatua zisizo za kulidhisha za kuhakikisha wadaiwa
sugu wa mikopo kutoka katika chama hicho wanarejesha mikopo hiyo.
Mmoja wa
wanachama hao Paulo Myinga alisema kuwa anashangazwa na kuona bodi ya chama
hicho cha Madibira Saccos inashindwa kuwachukulia hatua watu wanaoshindwa
kurejesha mikopo hiyo kwa muda mrefu na hivyo kukwamisha juhudi na malengo ya
chama hicho katika kuwasaidia wanachama wengine.
‘’Kuna
wadaiwa sugu katika chama chetu ambao wamekuwa wakikwamisha malengo na jitihada
za wanachama wengine katika kufikia malengo ya maendeleo,ni wakati sasa kwa
viongozi waliopewa dhamana ndania ya chama hicho kuongeza ukali katika
kukusanya madeni’’alisema Myinga.
Akijibu
tuhuma hizo,Meneja wa Madibira Saccos Henry Mdapo alisema kuwa kutokana na
chama kubaini kuwepo kwa baadhi ya wanachama wasiowaaminifu katika susla la
urejeshaji mikopo,uongozi wa chama hicho umesha weka mikakati ya kuhakikisha
fedha zote zinazodaiwa zinarejeshwa.
Alisema
mbali na uongozi huo kuwaita kwa busara wanachama wanaodaiwa kwa lengo la kurejesha
mikopo wanayodaiwa,lakini pia uongozi huo umeshaingia makubaliano na kampuni ya
Majembe Action Mart ambayo itatumika kukusanya madeni yote kutoka kwa wadaiwa
sugu.
Aidha
alibainisha kuwa ni asilimia 64.60 tu ya mikopo ya kilimo ndiyo iliyokuwa
imerejeshwa kwa mwaka huu na kuwa uamuzi wa kutumia viongozi wa
vitongoji,vijiji na kampuni ya ukusanyaji wa madeni ya Majembe Action Mart
itasaidia kurejesha madeni hayo.
Mbali na
uamuzi huo,Meneo huyo alisema kuwa wanachama mbalimbali wamekuwa wakipewa elimu
ya matumizi bora ya mikopo kabla ya kukopa na kuwa wadaiwa wote wamekuwa
wakikaidi kurejesha mikopo na kusababisha usumbufu kutokana na sababu zisizo na
msingi.
Kwa upande
wake,Mwenyekiti wa chama hicho cha Madibira Saccos Athuman Kinyangasi alisema
kuwa uongozi wa chama hicho hauwezi kuwafumbia macho wanachama ambao
wameshindwa kurejesha mikopo kwa wakati na kuwa mpaka sasa kuna mikakati
madhubuti ya kukusanya madeni yote ya chama hicho.
‘’ni lazima
tukusanye madeni yote ya chama kutoka kwa wadaiwa sugu ili kuwapa fursa
wanachama wengine kukopa kwajili ya shughuri mbalimbali za kimaendeleo zikiwemo
kilimo na biashara’’alisema kinyangasi.
Kwa mjibu wa
taarifa kutoka kwa mwenyekiyi wa Kamati ya usimamizi ya Madibira Saccos,Said
Kilawa ni kuwa chama hicho kinadai kiasi cha sh bilioni 1,142,053,743 na kuwa
fedha zilizorejeshwa mpaka sasa ni kiasi cha sh 310,407,367. Ambazo ni sawa na
asilimia 21.4.