Wajumbe wa dawati hilo
wapo katika ziara ya kutembelea vituo mbalimbali ikiwa ni katika
maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kiijinsia
Mmoja wa wajumbe wa dawati la Ukatili na Unyanyasaji wa kijinsia la
polisi mkoa wa Mbeya Mary Gumbo akikabidhi zawadi ya sabuni kwa watoto
yatima waishio katika kituo cha Malezi na Matunzo ya watoto Yatima cha
Msamaria Mwema kilichopo Songwe wilayani Mbeya
Mkuu wa Dawati la Ukatili na Unyanyasaji wa kijinsia la polisi mkoa wa Mbeya mkaguzi msaidizi wa jeshi hilo Samora Saranga aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Malezi na Matunzo ya watoto Yatima cha Msamaria Mwema kilichopo Songwe wilayani Mbeya.
Saranga aliyeambatana na wajumbe wengine wa dawati hilo kutembelea kituo hicho alisema watoto yatima wanapaswa kutambua kuwa maisha wanayoishia yapo katika mipango ya mwenyezi Mungu na si wao wala wazazi wao waliopenda jamii hiyo iishi hivyo.
Ziara ya wajumbe wa dawati hilo kituoni hapo ni mwendelezo wa ziara katika vituo mbalimbali ikiwa ni katika kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
Na Lyamba Lya Mfipa