Wanahabari toka Ubelgiji wapo nchini kumfuatilia Samatta

Waandishi wawili wa habari wamesafiri kutoka Ubelgiji kuja nchini kwa ajaili ya kumfuatilia mshambuliaji wa kimataifa Mbwana Samatta anaecheza kwenye klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji.
Gauyentie Bogouet pamoja na Marc Cornelissen ambao wanaandikia gazeti la Het Belang van Limburg na website ya http://www.HBVL.BE wana siku tatu tangu wafike Tanzania na leo watatembelea familia ya Mbwana Samatta.
Lengo kuu la safari yao ni kutaka kujua kwa undani alipotoka Samatta njia alizopita kabla ya kutua Genk maisha na tamaduni za taifa anakotokea.
“Tupo hapa kwa siku mbili sasa (jana) tumekuja kwa ajili ya kutaka kujua zaidi kuhusu Samatta alipotoka alikopita na namna alivyofanikiwa kufika Genk. Kesho (leo) tutatembelea nyumbani kwao kwa ajili ya kukutana na familia yake,” alisema Cornelissen mara baada ya kumalizika kwa mechi ya Tanzania vs Lesotho.
Waandishi hao walikuwepo kwenye mechi kati ya Stars dhidi ya Lesotho na walishuhudia Mbwana Samatta akifunga goli katika mchezo huo uliomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.
Huenda ziara yao ikawa na faida kwa wachezaji wa Tanzania kwa sababu wamepata fursa ya kushuhudia mechi na kuwaona baadhi ya wachezaji wakiwa katika kiwango bora katika mchezo huo hivyo huenda katika ripoti yao wakashauri vilabu vya Ubelgiji kuja Tanzania kusaka vipaji.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2t8wivC
via IFTTT