Showing posts with label June 04. Show all posts
Showing posts with label June 04. Show all posts
Daktari atuhumiwa kuwapa mimba wanawake 60 bila wenyewe kujua

Daktari atuhumiwa kuwapa mimba wanawake 60 bila wenyewe kujua

Mahakama moja nchini Uholanzi imeidhinisha ombi la familia zinazotaka vipimo vya vinasaba DNA vichukuliwe juu ya mmiliki wa kliniki ya uzazi ya daktari anayeshutumiwa kutumia mbegu zake za kiume katika makumi kadhaa ya kesi.
Jan Karbaat anatuhumiwa kuwa baba wa watoto wapatao 60 katika kituo cha afya alichomiliki katika eneo la Bijdorp, karibu na Rotterdam.
Vipimo sasa vitafanyika juu ya vifaa vilivyochukuliwa kutoka kwenye nyumba yake baada ya kifo chake mwezi Aprili, akiwa na umri wa miaka 89.
Wakili wa familia yake anasema hakuna ushahidi wa kuthibitisha madai hayo.
Jan Karbaat alijiita “Muasisi wa fani ya uzazi wa kusaidiwa”.
Kliniki yake ilifungwa mwaka 2009 wakati kulikuwa na taarifa kwamba alidaiwa kugushi data, uchunguzi na maelezo ya watoaji wa mbegu za kiumena kuzidisha idadi inayoruhusiwa ya idadi ya watoto sita kwa kila anayejitolea kutoa mbegu za uzazi.
Katika kesi ya mahakamani mwezi uliopita, wakili wa wazazi 22 na watoto walisema kwamba visa vinavyoshukiwa vinajumuisha mtoto wa mteja wao mwenye macho ya hudhurungi wakati alikuwa na macho ya blu na mvulana wa mteja wakeambaye anasura inayofanana na daktari.
Taarifa za vinasaba DNA zitasalia kuwa siri hadi pale watoto watakapoonyesha kuwa kuna sababu za kuamini daktari alikuwa baba yao, kulingana na mwandishi wa BBC Anna Holligan, ambaye alikuwa katika mahakama ya wilaya ya Rotterdam.
Hatimae, kama taarifa za vinasaba-DNA zitawiana na watoto hao ambao wengi wao walizaliwa miaka ya 1980s, kutakuwa na tumaini la kumshitaki daktari, labda kwa misingi ya kwamba hawangepaswa kuwepo, ameongeza Anna Holligan.
Joey, ambaye anaamini Jan Karbaat huenda ni baba yake ameiambia BBC: ” Ina maana kubwa kwangu … Tunatumai kupata majibu .”
Wakili wa familia ya Karbaat anapinga kufanyika kwa vipimo vyovyote vya vinasaba DNA.
Wakati wa uhai wake, daktari mwenyewe alikataa kufanya vipimo hivyo.
Hata hivyo, mwezi uliopita,kijana yake Jan Karbaat alitoa vinasaba vyake DNA vipimwe ambavyo vilionyesha kuwa daktari anaweza kuwa baba wa watoto 19, waliozaliwa kwa njia ya uzazi wa kutungishwa mbegu kwa lugha ya kitaaamu IVF, kulingana na ripoti ya shirika la habari la AFP.

from Blogger http://ift.tt/2rGfgaG
via IFTTT


Jinsi ya Kumtambua Anayekupigia Kwenye Simu yako Kwa Jina na Mahali Alipo

Jinsi ya Kumtambua Anayekupigia Kwenye Simu yako Kwa Jina na Mahali Alipo

Leo nitakuonesha hatua ambazo zitakusaidia wewe kumfahamu nani anayekupigia kwenye simu yako na wapi anapotokea. Utaweza kufahamu kama simu hiyo inatoka kwenye kampuni au ni watu wanaosumbua. Nimeandalia njia mbili ambazo zitakusaidia kufuatilia namba ya simu kwa jina na mahala inapotokea.
Namba ngeni na binafsi ni moja kati ya vitu vinavyotisha katika maisha yetu ya kila siku unakutana na namba binafsi ambayo siyo ya kawaida tofauti kabisa na tulizozizoea.
Namba nyingi ambazo zinakuwa tofauti mara nyingi hutoka kwa makampuni ya kutafuta masoko kwa njia ya simu ili kutangaza bidhaa au huduma za wateja wao mbali mbali ambazo unaweza ukazipenda au usizipende. au namba ya mtu ambaye haipo katika simu.
Zifuatazo ni njia ambazo zinatumika kutambua namba ya simu ambayo imeingia kwenye simu yako ambapo utaweza kutambua jina na mahala alipo mtu anayekupigia.
Kutumia tovuti ya Truecaller
Hatua ya 1. Fungua tovuti ya Truecaller kwenye pc.
Tovuti ya Truecaller
Hatua ya 2. Chagua nchi ambayo unatokea kwenye orodha kama unatokea Tanzania chagua hapo kisha andika namba ya simu ya mtu ambaye unataka kumfahamu halafu bonyeza search.
tovuti ya Truecaller
Hatua ya 3. Kitatokea kiboksi ambacho kinakutaka ujiunge na true caller ili kuweza kupata taarifa za namba uliyo andika. Kama una account ya Gmail unaweza ukaitumia, au unaweza ukajiunganisha nao kwa kupitia account yako ya facebook kwa urahisi zaidi chagua kisha endelea.
Chagua njia za kujisajili ili kupata matokeo unayotafuta
Baada ya kumaliza usajili utapewa taarifa zote za namba uliyoandika ikiwa ni jina pamoja na mahali alipo. Taarifa hizo zinakuwa ni kweli kwa 90%.
Truecaller itakuletea taarifa za namba ya mhusika kama jina na mahala alipo
Hiyo ndiyo ilikuwa njia rahisi ya kufahamu namba ngeni kwa kutumia tovuti ya True caller. Nadhani kuanzia sasa hakuna namba ngeni mpya tena shikamoo Truecaller.
Kutumia App ya Truecaller kwenye simu yako
Unachotakiwa kufanya fungua playstore kisha pakua app ya Truecaller halafu install kwenye simu yako.
Hatua ya 1. Pakua app ya Truecaller moja kwa moja kwenye simu yako kwa kubonyeza hapa hiyo link inayofuata >> Truecaller pakua hapa
Hatua ya 2. Baada ya kupakua Truecaller kwenye playstore fanya installation ya app hiyo kwenye simu yako kisha ifungue.
Muonekano wa app ya Truecaller
Hatua ya 3. Utaona sehemu ya kutafuta jina au namba, tofauti na uzuri wa hii app haihitaji ujisajiri ili kuweza kupata taarifa za mtu unayetaka kumfahamu kama ilivyokuwa kwenye tovuti yake, kwa hiyo unaweza ukaandika namba yake hapo kisha utaona jina na mahali alipo.

from Blogger http://ift.tt/2rFjBLc
via IFTTT


Mwanzilishi wa kampuni ya Alibaba Jack Ma aliwahi kuomba kazi katika makampuni 30 na kukataliwa kabla ya kuwa mtu tajiri zaidi China.

Mwanzilishi wa kampuni ya Alibaba Jack Ma aliwahi kuomba kazi katika makampuni 30 na kukataliwa kabla ya kuwa mtu tajiri zaidi China.

Jack Ma ni moja kati ya watu matajiri zaidi duniani akiwa na utajiri unaofikia dola bilioni 20.4, mtandao wake wa Alibaba kwa siku unaingiza watu milioni 100, ambapo unaunganisha wauzaji na wanunuzi kutoka sehemu mbali mbali duniani.
Ila kabla ya kuwa mtu tajiri zaidi China, Ma alipitia vikwazo vingi sana maishani mwake.
Katika mahojiano ya hivi karibuni na Charlie Rose, mfanyabiashara huyo alisema alishafeli mitihani ya kujiunga na vyuo mara tatu mfululizo.
Baada ya kuachana na chuo, Ma aliomba kazi kwenye makampuni 30 tofauti na kukataliwa.
“Niliwahi kwenda kuomba kazi ya kuwa askari polisi; waliniambia, ‘we haufahi,'”.”Pia niliwahi kwenda kuomba kazi katika mgahawa wa KFC walipofungua tawi lao karibu na mtaa wetu. Watu ishirini na nne tuliomba kazi pale. Kati ya watu hao ishirini na nne tulioomba kazi mimi peke yangu ndiye niliyekataliwa.” Alimwambia Rose.
Wakati anaanzisha mtandao wa Alibaba mwaka 1998, Ma alikutana na vikwazo vingi sana.
Mtandao wake huo haukuweza kumuingizia kipato kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo kutokana na mabenki kutokuwa tayari kufanya kazi na Ma hivyo njia za malipo katika mtandao huo zilikuwa ni ngumu.
Ma aliamua kuja na njia mbadala ya malipo katika mtandao wake huo iliyoitwa Alipay. Programu hiyo ilikuwa inawezesha wauzaji na wanunuzi kutoka mataifa mbali mbali kuweza kutumiana pesa kwa njia nyepesi zaidi.
“Watu wengi nilikuwa nikiwaambia kuhusu Alipay, waliniambia, “Hilo ni wazo la kijinga kuwahi kufikiriwa na wewe,'”alisema Ma.”Mimi sikujari kama wao walisema ni wazo la kijinga cha msingi ni kwamba watu wataweza kutumia mfumo huo basi.”
Leo hii, watu milioni 800 wanatumia mfumo wa Alipay kufanya manunuzi katika mtandao wa Alibaba.

from Blogger http://ift.tt/2rxviSs
via IFTTT


Jeshi la polisi Dubai kuanza kutumia gari za umeme kutoka BMW

Jeshi la polisi Dubai kuanza kutumia gari za umeme kutoka BMW

Jeshi la polisi jijini Dubai wameongeza gari mpya za BMW i3 ambazo zinatumia umeme kwenye orodha ya gari zao, Jeshi la polisi Dubai linafahamika ulimwenguni kwa kuwa na gari za kisasa na zenye gharama kubwa sana.
Gari kama Ferrari, Mercedes Benz, Bugatti Veyron, Aston Martin, Bentley, McLaren ni aina ya magari ambayo yanamilikiwa na jeshi la polisi jijini Dubai, ila idadi kubwa ya magari hayo hayatumiki kwa kufukuzia wahalifu bali ni kwa maonesho.
Gari hiyo ya BMW i3 ambayo inatumia umeme ilioneshwa kwa mara ya kwanza kwenye maonesho ya magari jijini humo, ambapo wazili wa nishati wa jiji hilo Al-Mazrouei alisema wanampango wa kuongeza magari mengi zaidi yanayotumia umeme katika jeshi la polisi la Dubai kwa asilimia 10 ya magari yote ya serikali ambapo matumizi ya magari hayo ya umeme yatasaidia kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa unaosababishwa na gari zinazotumia mafuta kwa asilimia 15 ndani ya miaka 4 ijayo.
Jeshi la polisi nchini Marekani, Ujerumani, Italia, Australia na Uingereza tayari nao wameshaanza kutumia gari hizo za BMW i3 kwenye majeshi yao ya polisi.

from Blogger http://ift.tt/2sDdPaw
via IFTTT


Kategori

Kategori