Jack Ma ni moja kati ya watu matajiri zaidi duniani akiwa na utajiri unaofikia dola bilioni 20.4, mtandao wake wa Alibaba kwa siku unaingiza watu milioni 100, ambapo unaunganisha wauzaji na wanunuzi kutoka sehemu mbali mbali duniani.
Ila kabla ya kuwa mtu tajiri zaidi China, Ma alipitia vikwazo vingi sana maishani mwake.
Katika mahojiano ya hivi karibuni na Charlie Rose, mfanyabiashara huyo alisema alishafeli mitihani ya kujiunga na vyuo mara tatu mfululizo.
Baada ya kuachana na chuo, Ma aliomba kazi kwenye makampuni 30 tofauti na kukataliwa.
“Niliwahi kwenda kuomba kazi ya kuwa askari polisi; waliniambia, ‘we haufahi,'”.”Pia niliwahi kwenda kuomba kazi katika mgahawa wa KFC walipofungua tawi lao karibu na mtaa wetu. Watu ishirini na nne tuliomba kazi pale. Kati ya watu hao ishirini na nne tulioomba kazi mimi peke yangu ndiye niliyekataliwa.” Alimwambia Rose.
Wakati anaanzisha mtandao wa Alibaba mwaka 1998, Ma alikutana na vikwazo vingi sana.
Mtandao wake huo haukuweza kumuingizia kipato kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo kutokana na mabenki kutokuwa tayari kufanya kazi na Ma hivyo njia za malipo katika mtandao huo zilikuwa ni ngumu.
Ma aliamua kuja na njia mbadala ya malipo katika mtandao wake huo iliyoitwa Alipay. Programu hiyo ilikuwa inawezesha wauzaji na wanunuzi kutoka mataifa mbali mbali kuweza kutumiana pesa kwa njia nyepesi zaidi.
“Watu wengi nilikuwa nikiwaambia kuhusu Alipay, waliniambia, “Hilo ni wazo la kijinga kuwahi kufikiriwa na wewe,'”alisema Ma.”Mimi sikujari kama wao walisema ni wazo la kijinga cha msingi ni kwamba watu wataweza kutumia mfumo huo basi.”
Leo hii, watu milioni 800 wanatumia mfumo wa Alipay kufanya manunuzi katika mtandao wa Alibaba.
from Blogger http://ift.tt/2rxviSs
via IFTTT