VIJANA nchini wametakiwa kuendeleza kujiandikisha katika
Daftari la kudumu la mpiga kura Kwa mfumo wa Kielekroniki (Bvr) na kutimiza
wajibu wao kwa kuchagua kiongozi kama watu wenye hekima.
Wito huo umetolewa mbele ya maelfu ya vijana kutoka sehemu mbalimbali
nchini katika kongamano la vijana wa Katoriki Tanzania la kila mwaka
linalofanyika Mkoani Njombe na Askofu wa jimbo la Mpanda, Gervas Nyaisonga
mjini hapa jana.
Askofu Nyaisonga amesema kuwa vijana wanaotakiwa watumie
wajibu wao wa kupiga kura na wajiazari kutumika katika kipindi hiki cha
uchaguzi.
Alisema “Vijana mmekuwa mkitumika katika mambo mbalimbali
hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi kwa namna ya maandamano na wengine
kufanywa uraghai ili kupitisha kiongozi asiyefaa, angalieni na epukeni watu wa
aina hiyo ili kupata viongozi bora,”
Alisema anajua kwa mkoa wa Njombe zoezi limeshapita lakini
kwa mikoa ambayo zoezi linaendelea wajitokeze kujiandikisha ili kutumia hakiyao
ya msingi na kiimani kumchagua kiongozi bora na kuwa katika sarafu inapande
mbili za upande wa Kaisali na upande wa dini.
“Najua tu uchaguzi utakuwa jumapili na vijana wengi najua
mnapenda kusali lakini siku hiyo muhakikishe mnawahi kanisani katika misa ya
asubuhi na kwenda kupiga kura hatakama foleni itakuwa ndefu mvumilie si
mshawahi kufunga siku hiyo mtafunga,” alisema Askofu Nyaisonga.
Alisema kuwa vijana wanawajibu mkubwa wa kupigia kura
kiongozi wanae mtaka lakini kwa kujiandikisha wanaweza kufanya hivyo kama
hawata jiandikisha ni sawa na kazi bure hivyo amewataka kwa ambao zoezi la
uandikishaji unaendelea wajiandikishe katika dafdari hilo ili kupata fulsa ya
kupiga kura.
Aliwataka vijana kutumia uchaguzi huo kama watu wenye hekima
na watu wenye macho na kutumia hekima ya Mungu kufanya uchaguzi wa mtu wanaye
mtaka bila kupenda pesa za mgombea yeyote.
Aliongeza kuwa ameisikia tume imesema imefanikiwa katika
uandikishaji wa Daftari la kudumu la mpiga kula lakini anashangaa haijasema
imefanikiwa kwa kuwaandikisha watu wangapi na kuwa angefurahi kusikia
imefanikiwa kuwandikisha watu 45 milioni.
“Vijana kama hamtajiandikisha unatumika katika maandamano
kwa hiyo jiandikisheni na mkapige kura, suala la Katiba Pendekezwa lilikuwa zinazungumziwa
sana lakini sasa limesubilishwa wote tupo kimya wote wanazungumzia na walio
kuwa hawazungumzii wote tupo sawa” alisema Askofu Nyaisongo