WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa - Tanzania Benald
Membe amesema kuwa Watanzania wawe makini kwa na watu wenye kashifa za wizi na
ataibadilisha Tanzania na kuhakikisha mkoa wa Njombe unauza viazi katika
majeshi ya nchi za Ulaya.
Amesema kuwa atahakikisha kuwa Tanzania inakuwa ya amani na
kuhakikisha Watanzania wananufaika na mazao yao kwa kuhakikisha anawaunganisha Watanzania
na soko la viazi la nje.
Amesema kuwa viazi hivyo vinahitajika sana katika majeshi ya
Ulaya yanatumia chips za viazi kwa ajili ya kula wakati wanaenda vitani
kutokana na ukavu wake.
Amesema Watanzania waangalie watangaza nia ambao watakuja
wasije wakawarubuni na kuwa wengi wanao taka uraisi si wasafi hivyo wahakikishe
wanachagua mtu msafi ambaye ataliimalisha taifa.
Aidha membe amesema kuwa ajajitahidu kuhakikisha mambi ya
ujambazi yanatoweka hapa nchini, na kuwa ataimarisha ulinzi wa mipaka ya Tanzania
na kuwafanya Watanzania kuwa huru kutokan ana matishio mbalimbali ya ugaidi.