Papa Francis ameidhinisha kuundwa kwa idara mpya itakayokuwa na mamlaka ya kuwawajibisha maaskofu wa kanisa katoliki wanaokosa kuwachukulia hatua wale waliochini ya usimamizi wao, wanaotuhumiwa kuwanyanyasa watoto kingono .
Mabadiliko hayo yanafanyika baada ya malalamiko mengi kutolewa na waathiriwa wa vitendo hivyo dhalimu.
Jopo la viongozi wa kanisa hilo pia walikuwa wamependekeza hilo.
Sheria za dini hiyo, ziitwazo Canon law zilikuwa zimetoa mwongozo wa hatua gani zichukuliwe dhidi ya maaskofu wanaotelekeza wajibu wao lakini uongozi wa Vatican haujawachukulia hatua wale wanaofumbia macho makosa ya unyanyasaji wa kingono unaofanyika katika maeneo yao.