Maamuzi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuhusu Rufaa za Wabunge na Madiwani



Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepokea jumla ya rufaa 54 za Wabunge
kupinga Maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi katika majimbo mbalimbali nchini. Pia
jumla ya rufaa 200 za madiwani
kutoka kwenye kata za Halmashauri mbalimbali.


Tume inaendelea kupitia vielelezo vilivyowasilishwa na Wagombea
(warufani) na Wasimamizi wa Uchaguzi kutoka Halmashauri mbalimbali. Pia imeanza
kuzitolewa maamuzi rufaa za Wabunge tarehe 31/8/2015.  Leo tarehe 01/9/2015 zimejadiliwa na
kuamuliwa rufaa za Madiwani 53. 


Kati ya Rufaa hizo Rufaa za kupinga kuenguliwa zilikuwa 9 na Tume
imewarejesha wagombea Udiwani 8 na mmoja (1) Tume imetoa maamuzi kuwa
kutenguliwa kwake ni sahihi. 


Aidha, Rufaa 44 zilikuwa za kupinga maamuzi ya
Wasimamizi wa Uchaguzi na zote Tume imezitolea maamuzi ya kuridhika na maamuzi
ya wasimamizi wa Uchaguzi. Hivyo, Rufaa 44 zimekataliwa na wagombea wataendelea
na kampeni zao.


Tume
inaendelea na vikao vya kusikiliza na kuamua
Rufaa zilizosalia na itakuwa inatoa taarifa mara kwa mara.

By Michuzi Blog