BAADA ya kupata matokeo mabovu kwa muda mrefu timu ya Njombe mji
imeamua kutafuta mwalimu mkuu wa timi ambaye amewasili hii leo na kuahidi
matokeo ya kuwepo kwake kuanza kuonekana katika mechi ya kesho baina ya timu ya
Njombe mji na Mbeya city.
Kocha Mkuu wa Njombe Mji
Ally Bushiri amesema kuwa mashabiki wa timu ya Njombe mji waanze
kutaraji matokeo katika mchezo wake wa kwanza kuwa na timu hiyo na kuwa kwa
michezo iliyo baki ni lazima ataifikisha timu hiyo sehemu mzuri.
Mwenyekiti wa timu hiyo Erasto Mpete amesema kuwa wakati huu
mgumu ndio wa mashabiki kuonyesha kwa timu hiyo kwa kuwa matokeo inayo pitia
wanataraji mabadiliko kama watakuwa na ushirikiano.
Pamoja na uongozi kuwa na matumaini hata kwa mashabiki huku kuhusu
wakati wa ujio wa kocha ikiwa ni wakati wake muafaka.
Timu
ya Njombe mji sasa ipo katika nafasi ya mkiani lakini bado wanamichezo mingi
ambayo kama wakifanya vizuri watakuwa katika nafasi nzuri.