Elimtaa Tv Njombe Mji Kukipiga na Singina United uzinduzi uwanja wa sabasaba Njombe

Uwanja umekamilika ni ule wa sabasaba wa nyumbani kwa Njombe Mji FC
UWANJA WA SABASABA NJOMBE

UWANJA wa sabasaba wa mjini Njombe unatarajiwa kufanyiwa majaribio Jumapili wiki hii kwa kucheza mechi ya kujipima uwezo kati ya timu ya Njombe Mji wenyeji na Timu ya Singida United ya mkoani singida zote zikiwa zinaingia ligi kuu Tanzania bara msimu huu.
Meneja wa uwanja wa Sabasaba anasema kuwa mechi hiyo itakuwa ni yakwanza kuzikanjaka nyasi hizo na kuwa kama uzinduzi wa uwanja huo na kuangalia mapungufu katika miundombinu yake.
Katibu wa CCM wamiliki wa uwanja huo anasema kuwa uwanja huo umekamilika kwa asilimia kubwa na mechi hiyo itasaidia kuona mapungufu yaliyo salia na kuyakamilisha kabla ya kuingia Ligi kuu.
Mashabiki nao wanasema wamefurahishwa na uwaja kufikia hatua hiyo na kusema kuwa hamu yao ni kuona wachezaji wakubwa wakicheza mkoani Njombe.

Timu hizo mbili zote zimepada dalaja msimu uliopita na kuingia ligi kuu mwaka huu pamoja na timu Lipuli ya mkoani Iringa.