Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh Abdallah Kigoda (pichani) amefariki dunia jioni hii nchini India alikokuwa anapatiwa matibabu.
Taarifa za kifo cha Mh Kigoda ambaye pia alikuwa mbunge wa Handeni mkoani Tanga zimethibitishwa na ofisi ya Bunge jijini Dar es Salaam.
Mhe. Dkt. Kigoda alikwenda nchini India kwa matibabu tarehe 18 Septemba, 2015, kupata matibabu katika hospitali Hiyo ya Apollo. Taarifa zaidi kutolewa baadaye.
Modewji Blog inaungana na Familia ya Marehemu pamoja na Watanzania kwa ujumla katika kuomboleza kifo cha Dkt. Kigoda, Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amen.