LOWASSA ATIKISA JIJI LA MWANZA WANANCHI ZAIDI YA 130 WAZIMIA KWENYE MKUTANO WAKE VIWANJA VYA FURAHISHA


Jiji la kibiashara la Mwanza limejikuta likisimamisha shughuli zake zote kupisha mkutano mkubwa wa hadhara uliokuwa ukiongozwa na mgombea urais wa Chadema anayeungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA Edward Lowassa huku zaidi ya wananchi 130 wakizimia.


Kishindo cha mgombea huyo wa nafasi ya urais Edward Lowassa ndani ya uwanja wa Furahisha kikatikisa afya za wakazi wa jiji la Mwanza kwa mujibu wa chama cha msalaba mwekundu.

Akiwa jiji Mwanza alikuwa na kazi rahisi zaidi ya kuomba kupigiwa kura ya ushindi wa kishindo kwakuwa anania, ari na nguvu za kuhakikisha Tanzania inapata uchumi imara huku akiwataka watanzania kujiandaa vema na Oct 25 mwaka huu.



Mhe. Edward Ngoyai Lowassa na Highness Kiwia wakiwasili viwanja vya Furahisha Mwanza,leo Jumatatu 12/10/2015