Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amezungumza na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa Kulevya Bw. Rogers William Siyanga ambaye amemhakikishia kuwa kazi ya kukabiliana na tatizo la biashara na matumizi ya dawa za kulevya inaendelea vizuri.
Bw. Rogers William Siyanga amesema tatizo la dawa za kulevya lilikuwa kubwa na ametaja dawa za kulevya ambazo Mamlaka inapambana nazo kuwa ni bangi, heroine, cocaine, kemikali bashirifu na kwamba kwa sasa imeanza kukamata na kuharibu mashamba ya bangi na bangi iliyovunwa.
Amebainisha mikakati mitatu inayotumika katika mapambano dhidi ya tatizo hilo kuwa ni kuzuia dawa za kulevya zisiingie nchini, kutoa elimu kuanzia shule za msingi, sekondari, vyuo na kwenye jamii ili watu waache kutumia dawa za kulevya na kutoa tiba kwa watu walioathirika na dawa za kulevya, na pia ametoa wito kwa watu wenye waathirika wa dawa za kulevya kuwapeleka katika mamlaka hiyo ili watibiwe.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
23 Agosti, 2017
from Blogger http://ift.tt/2ipaI5F
via IFTTT