Tuache siasa za kipuuzi puuzi- Zitto

Niseme jambo moja muhimu Sana. Miswada ya sheria za madini tunazopitisha wiki hii ni hatua za kimapinduzi na kiokombozi. Sio hatua ndogo. Ni hatua zenye maumivu. Hata hivyo tukiweka mikakati ya kukabili changamoto zitakazoanza kutukabili maumivu yatakuwa ya muda mfupi tu.
Hivyo, tusijidanganye kuwa kila kitu kitakuwa ‘ mswano ‘, la hasha. Kampuni za nje zinazoweka mitaji yao hapa Tanzania zitaacha kuweka mitaji na zingine zitaondoa mitaji yao. Uzalishaji wa Dhahabu utashuka na Kwa kuwa dhahabu inachangia 30% ya Fedha za kigeni tutatetereka kidogo upande wa urari wa biashara na hata shilingi yetu kushuka thamani.
Serikali inapaswa kuweka mikakati ya muda wa kati kukabiliana na changamoto hizi. Moja ya njia muhimu na yenye maana kubwa ni kuongeza mauzo nje kwenye sekta ya kilimo ( Korosho, Katani, Kahawa, Chai, Pamba). Pia mauzo nje ya bidhaa za viwanda. Uzalishaji wa Sukari na Mawese ghafi unapaswa kuongezeka ndani ya wa kati ili kuokoa matumizi ya fedha za kigeni kununua bidhaa hizo nje.
Tutashambuliwa Sana na propaganda za magazeti ya ubepari mamboleo ( neo liberal right wing media). Hivyo, viongozi wetu wa kisiasa WANAPASWA kuwa WAMOJA kwenye shabaha hata kama wanapingana kwenye njia. Vyombo vya habari vya ndani vinapaswa kuandaliwa kuelewa hali yetu na kuelewesha dunia.
Huu sio wakati wa siasa za kipuuzi puuzi, ni wakati wa Siasa za kiuongozi.
Tukisimama imara na pamoja Kwa ushirikiano tutavuka katika kujenga Uchumi shirikishi wenye kuzalisha ajira nyingi. Tukiendekeza kuzodoana, kutukanana, kugandamiza demokrasia na kukomoana, ninawaapia tutashindwa vita Hii.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2uFQ56p
via IFTTT