Showing posts with label July 04. Show all posts
Showing posts with label July 04. Show all posts
MADUKA ya Supermarkets za Nakumatt Hali Tete..

MADUKA ya Supermarkets za Nakumatt Hali Tete..

Mamia ya wafanyakazi huenda wakakosa ajira Afrika Mashariki baada ya maduka ya jumla ya Nakumatt kuonekana kuwa hatarini.
Nakumatt iliyo na maduka nchini Kenya, Uganda, Tanzania na Rwanda inakabiliwa na changamoto za kulipa madeni yake, na sasa wadeni wake wanatishia kuweka mali ya Nakumatt kwenye mnada.
Kwa miaka kadhaa Nakumatt imejivunia kukidhi mahitaji yote ya wateja na kauli mbiu ya ‘You need it, we’ve got it’ (Unahitaji, Tunacho), lakini hivi karibuni hata bidhaa muhimu kama mkate zimekuwa nadra kupatikana kwenye rafu zake.
Wateja wa duka hilo la Jumla walitaka kutambua yanayojiri kwenye duka hilo kupitia mtandao baada ya kukosa bidhaa muhimu lakini wasimamizi wa maduka hayo wamekanusha madai kwamba huenda biashara yake ikaporomoka.
Pindu tu baada ya habari kuanza kuenea mitandaoni, ilianza kubainika wazi kuwa maduka hilo haliwezi tena kuwalipa wanaoyauzia bidhaa.
Nakumatt pia inadaiwa kushindwa kulipa kodi ya majumba ambayo yanatumiwa kwa maduka yake.
Wiki moja tu baada ya kufunga maduka matatu nchini Uganda, madalali wametwaa mali ya Nakumatt kwenye jumba moja la kibiashara viunganimwa jiji la Nairobi, kwa madai ya kutolipwa kodi ya takriban dola nusu milioni.
Aidha kampuni hiyo inakabiliwa na kesi nyingine ya kufilisika kwa kutolipa deni la zaidi ya dola laki saba, na kwa kuandika cheki hewa.
Serikali ya Kenya imeingilia kati majadiliano baina ya duka hilo na wadeni wake, ili kupata suluhisho litakalozuia kampuni hiyo kusambaratika, haswa kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini Kenya mwezi Agosti.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2uldgn4
via IFTTT


Chid Benz Ageukia Kilimo

Chid Benz Ageukia Kilimo

Baada ya kukaa nje ya game la bongo fleva kwa muda, Rapa Chidi Benz amefunguka na kusema ameamua kujikita kwenye killimo akishirikiana na mama yake mzazi ili kuweza kujikimu kimaisha.
Leo akiwa kwenye dakika 10 za maangamizi kipindi cha Planet Bongo ndani ya East Afrca Radio Chidi amesema kwamba mama yake ni mtu wake wa kwanza kwenye kumpatia sapoti ndiyo maana anashirikiana naye katika kuwajibika kiuchumi.
“Kwa sasa najishughulisha na kilimo kwa sana. Mimi na mama yangu tuna mashamba huko Chanika kwa hiyo hichi kipindi nilichokaa nje ya ‘game’ kilimo kinaendeleza maisha yetu japokuwa mimi mkulima wa mjini’, alisema Chidi.
Aidha Chidi ameongeza kwamba :
“Lakini nina familia niliyoitengeneza kipindi nafanya vizuri kwenye game kwa hiyo siwezi nikafa na njaa wakati mimi nilikuwa nawalea na kuwasaidia pale walipokuwa wakinihitaji. Wasanii wengi wapo upande wangu hawakumbuki mabaya yangu wengi wanarudisha mawazo yao nyuma kwa mazuri yangu”,Chidi Benz aliongeza.
Hata hivyo rapa huyo kwa sasa amerudi na ngoma aliyomshirikisha Mkongwe Q- Chillah inayokwenda kwa jina la ‘muda’.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2uFD3pr
via IFTTT


Idris Sultan Apata Shavu la Kucheza Movie Hollywood Marekani

Idris Sultan Apata Shavu la Kucheza Movie Hollywood Marekani

Baada ya wiki ya mchakato wa usahili, Mshindi wa Big Brother Africa-Hotshots wa 2014, Idris Sultan ataonekana katika filamu ya ‘Ballin …On the Other Side of the World,’ itayoandaliwa nchini Marekani chini ya muongozaji Harvey White.
Muongozaji wa filamu hiyo aliwahi kufanya kazi na wasanii wenye majina makubwa akiwemo Chris Brown, Mariah Carey, Lady Gaga na Tamia.
Akiwa kama mhariri wa filamu, amehariri baadhi ya filamu kama vile ‘Think Like A Man 2,’ ‘The Wedding Ringer,’ na ‘King of the Dance Hall’ akishirikiana na Whoopi Goldberg.
Hadithi ya filamu hiyo imetungwa na Torino Von Jones, ambapo hadithi hiyo inamhusu kijana mdogo wa Kenya (Kunjani), ambaye wazazi wake ni waathirika wa uhalifu uliojaa vurugu.
Siku moja katika maeneo ya ya shule, kijana huyo aliye na umri wa miaka kumi na tatu aligunduliwa na padri wa Kimarekani ambaye alimwona akicheza mpira wa kikapu na akaamini ana uwezo mkubwa na anaweza kushirikia ligi ya NBA.
Wote wawili waliendelea na urafiki wao na padri huyo alianza kumpatia ushauri. (King) itaigizwa na Sultan, ana haiba kubwa,lakini ni mhalifu mkubwa na hatari sana ambaye ana wazo jingine na anataka Kunjani kujiunga na kundi lake la wahalifu na atafanya kila liwezekanalo ili mpango huo ufanikiwe.
Mara ya mwisho Sultan alionekana katika filamu ya Tanzania ‘Kiumeni,’ ambayo itaoneshwa katika tamasha lijalo la wiki ya filamu la Zanzibar (ZIFF) ambapo ‘Kiumeni’ itaoneshwa wakati wa Siku ya tamasha ya filamu za Kiswahili ya ZIFF Julai 14, na mtayarishaji na nyota wa filamu Ernest Napoleon.
Mapema mwaka huu, Napoleon aliweka historia wakati alipochaguliwa kuwa rais wa kampuni ya uzalishaji na usambazaji wa filamu ya Marekani ya D Street Media Group yenye makao yake jijini New York, pamoja na ofisi katika miji ya Berlin, Buenos Aires na Cape Town.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa D Street na mtayarishaji mtendaji Dexter Davis walimtambua Idris kutokana na kuiangalia filamu ya “Kiumeni’.
“Idris Sultan has what it takes to become an international star and our upcoming film ‘Ballin… On the Other Side of the World’ is a perfect fit. We’re considering Mr. Sultan for other movies as well, alisema Davis.
Kampuni hiyo ya filamu inaazimia kupiga picha sehemu za Marekani na Kenya na haitachelea kutafuta vipaji vingine kwa waigizaji wa Kenya na nchi nyingine za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania pale inapolazimu.
Filamu hiyo imeandaliwa kwa bajeti ya Dola za Marekani milioni tano.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2ukTQ1P
via IFTTT


MAITI yaokotwa Bwawani

MAITI yaokotwa Bwawani

Mwili wa mtu ambaye hajafahamika umeokotwa katika bwawa la maji lililopo Mtaa wa Nkende Shuleni katika Halmashauri ya Mji wa Tarime.
Hili ni tukio la tatu la watu kuuawa kisha miili yao kutupwa kwenye mabwawa ya maji katika kipindi cha miezi sita iliyopita. Hivi karibuni, mwili wa kijana ambaye alikuwa dereva wa bodaboda ulikutwa ukiwa umetupwa katika eneo hilo hilo.
Kamanda wa Mkoa wa Polisi Tarime/Rorya, Henry Mwaibambe, amethibitisha kuokotwa kwa mwili huo na kubainisha kuwa Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi ili kuwabaini watu wanafanya mauaji hayo.
Chareles Kisege, ambaye ni mwenyekiti wa mtaa wa Nkende Shuleni na James Nyangai mwenyekiti wa mtaa wa Kimusi, wamesema matukio hayo yamezusha hofu miongoni mwa wananchi wanaoishi katika maeneo hayo.
Wamitaka serikali kuchukua hatua za haraka kuwadhibiti wauaji hao.
Licha juhudi za wananchi kutaka kuuopoa mwili huo, zoezi hilo limekuwa zito na gumu kutokana na kukosa zana.
Hata hivyo, mwenyekiti wa chama cha waendesha bodaboda wilayani hapa, Samwel Kegoye, amesema ingawa taarifa zinaonyesha kuwa mtu huyo aliyeuawa ni dereva wa bodaboda, wao badoi hawajapata taarifa hizo rasmi.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2tEZdvr
via IFTTT


Kategori

Kategori