Mtwara yapiga hatua upatikanaji wa maji safi na salama


 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendegu akiwakaribisha wajumbe wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji iliyowasili mkoani humo kukagua miradi ya maji.
 Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Amina Makilagi akieleza lengo la ziara ya kamati hiyo mkoani Mtwara.
 Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Amina Makilagi, akizungumza na wanahabari kuhusu ziara ya kamati hiyo ambayo inahitimishwa leo wilayani Masasi mkoni Mtwara.
 Mhandisi wa Maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara John Msengi akiwasilisha taarifa ya mradi wa maji wa Nanyamba kwa wajumbe wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji iliyotembelea kukagua mradi huo.
 Mwenyekiti wa kijiji cha  Kibaoni kinachohudumiwa na Mradi wa Maji wa Nanyamba, Issa Bakari     akieleza jambo kwa wajumbe wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji iliyotembelea kukagua mradi huo.
 Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Amina Makilagi akipanda ngazi za tanki la maji la mradi wa Maji wa Nanyamba.
 Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Amina Makilagi akivuka kidaraja kuelekea kukagua tanki lingine la maji la mradi wa Maji wa Nanyamba.
 Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Amina Makilagi akikagua kisima cha maji ya mradi wa Maji wa Nanyamba.
 Afisa Mtendaji wa Mamlaka ya Mji wa Nanyamba, akitoa ufafanuzi kuhusu kisima cha mradi wa Maji wa Nanyamba.
 Msafara wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ukiwasili kwenye ofisi za wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara kukagua mradi wa Maji wa Matogoro.


 Mhandisi wa Maji Peter Malekia (katikati) akieleza jambo kwa Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Amina Makilagi na wataalamu wa Wizara ya Maji wakiwa chini ya tanki la maji la Mradi wa Maji wa Matogoro linaloweza kuhifadhi maji lita 100,000.
 Mhandisi wa Maji Peter Malekia, akieleza jambo kuhusu bomba la Mradi wa Maji wa Mteogoro wakati Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ilipokuwa ikikagua miundombinu ya mradi huo.
 Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Amina Makilagi akionja maji ya bomba la maji ya Mradi wa Maji wa Matogoro.
 Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Amina Makilagi akimpongeza mwenyekiti wa Kamati ya Maji ya Mradi wa Maji wa Matogoro Mzee Mwanya Natanga Bwanaheri.


 Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Amina Makilagi akizungumza na viongozi wa kijiji cha Matogoro na Mradi wa maji baada ya kukagua mradi huo.
Bibi Rukia Maulana mkazi wa Matogoro, akieleza jambo kwa Kamati Ndogo ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji iliyotembelea mradi wa Maji wa Matogoro. Picha zote na Hussein Makame, MAELEZO