Wazazi na walezi wa wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2015 wilayani Tandahimba mkoani mtwara ambao kwasasa wamekosa vituo wametakiwa kuendelea na maandalizi ya watoto wao huku halmashauri ikijizatiti kujenga shule mbili za sekondari kwa ajili ya uchaguzi wa pili ifikapo mwezi februari mwakani.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa halmashauri ya Tandahimba Abdallah Njovu wakati wa maandalizi ya ujenzi wa shule mbili za mwaminaki iliyopo kata ya kitama na nandonde kata ya tandahimba kufuatia ufaulu mzuri uliyopelekea wilaya yake kushika nafasi ya kwanza kimkoa ambapo kati ya wanafunzi 3504 waliyofaulu wanafunzi 280 wamekosa vituo.
