Shughuli za kuitafuta ndege ya AirAsia iliyopotea jana ikiwa na watu 162 ndani, zinaendelea leo.
Ndege hiyo iliyokuwa ikitokea kwenye mji wa Surabaya, Indonesia kuelekea Singapore, ilipoteza mawasiliano na kituo cha udhibiti wa safari za anga Jakarta, mara baada ya rubani kuomba kubadili njia ili kukwepa hali mbaya ya hewa.
Singapore imesema imetuma boti mbili za kijeshi kulisaidia jeshi la Indonesia kuitafuta ndege hiyo ya Airbus chapa A320-200, inayoendeshwa na shirika la ndege la AirAsia Indonesia, na imesema pia ndege ya kikosi cha jeshi la anga chapa C-130, jana ilishiriki kwenye utafutaji huo.
Kwa mujibu wa shirika hilo, rubani wa ndege hiyo ambaye ni raia wa Indonesia alikuwa na uzoefu, na ndege hiyo ilifanyiwa matengenezo katikati ya mwezi Novemba.
By Magic Fm on fb
