Maulid kitaifa kufanyika Korogwe Tanga

Baraza Kuu la Waislam Tanzania limesema sherehe za Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad S.A.W zinatarajia kufanyika Korogwe Mkoani Tanga Januari 3 -2015 sawa na mwezi 12 mfungo sita hijiriya siku ya jumamosi kuamkia jumapili.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum amesema jijini Dar es Salaam Maadhimisho hayo ya maulidi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad S.A.W yatafanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja na kuwataka waislam wajitokeze kwa wingi katika sherehe hizo.
Amesema Kauli mbiu ya maadhimisho ya Maulid ni Uislam ni Amani, Umoja na Mshikamano ambapo pia Baraza hilo litatumia siku hiyo kupongeza Hotuba ya Rais Kikwete aliyoitoa Dec 22 mwaka huu wakati akizungumza na taifa kupitia wazee wa mkoa wa Dar es Salaam juu ya sakata zima la Akaunti ya Escrow

Related Posts