SERIKALI ITAPAMBANA NA RUSHWA ILI KUJENGA JAMII YENYE MAADILI BORA KWA WATUMISHI


kijazi
Katibu Mkuu Kiongozi Mwandamizi Kijazi (mwenye koti la bluu) akiongoza matambezi ya hiari sehemu ya maadhimisho ya siku ya Maadili nchini yatakayofikia kileleni tarehe 10 Desemba 2016 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam na Matembeze hayo yamefanyika Leo jijini Dar es salaam kuanzia kwenye viwanja vya Karimjee na kufikia ukomo viwanja vya Mnazi Mmoja.
kijazi-1
Katibu Mkuu Kiongozi Mwandamizi John Kijazi( mwenye koti la bluu) akishiriki katika mazoezi ya viungo baada ya kumaliza matembezi ya hiari ambayo yamefanyika Leo jijini Dar es salaam.
kijazi-2
Katibu Mkuu Kiongozi Mwandamizi Balozi John Kijazi akiwahutubia washiriki wa matembezi ya hiari ( hawapo pichani) mara baada ya kumaliza matembezi hayo Jijini Dar es salaam.
kijazi-3
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Profesa Musa Assad akizungumza mbele ya mgeni rasmi Balozi John Kijazi (hayupo Pichani) mara baada ya kumalizika kwa matembezi ya hiari katika viwanja vya Mnazi Mmoja na kushoto ni Katibu Mkuu wa Ikulu Peter Ilomo.
kijazi-4
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU) ambaye ni mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Maadhimisho ya Haki za Binadamu,Bw.Valentino Mlowola akifafanua jambo mara baada ya kumalizika kwa Matembezi ya Hiari yaliyomalizikia viwanja vya Mnazi Mmoja katikati ni Katibu Mkuu Balozi Kijazi.
kijazi-6
Kaimu Kamishna wa Maadili Bw.Waziri Kipacha akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Balozi John Kijazi kwenye Matembezi ya Hiari baada ya kumaliza.
kijazi-7
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi ( Mwenye koti la bluu) akiwa kwenye picha ya pamoja nabaadhi ya viongozi na watumishi kutoka Taasisi zinazosimamia Maadili,Uwajibikaji,Utawala Bora,Haki za Binadamu na Mapambano dhidi ya Rushwa baada ya kumalizika kwa matembezi ya Hiari ambayo ni sehemu za Maadhimisho ya Siku ya Maadili nchini yanayotarajia kufikia kileleni Desemba 10,2016 viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
kijazi-8
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Kijazi (mwenye koti la bluu) akiwa katika picha ya pamoja na watoto ambao waliungana na watumishi katika Matembezi hayo yaliyofanyika Leo.
Picha Zote na Ally Mataula-Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
...........................................................
Na Alex Mathias na Joseph Ishengoma
Serikali ya awamu ya tano imesema kuwa imedhamiria kwa dhati kupambana na rushwa za kila aina ili kujenga jamii yenye maadili na inayochukia vitendo vya rushwa kwa kufuata kauli ya Rais wa Tanzania anayekemia Rushwa nchini.
Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Mwandisi Balozi John Kijazi amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akihitimisha matembezi ya watumishi wa taasisi zinazosimamia maadili, uwajibikaji, utawala bora, haki za binadamu na mapambano dhidi ya rushwa yaliyoanza mapema Asubuhi katika viwanja vya Karimjee na kufikia mwisho viwanja vya Mnazi Mmoja ambayo yaliweza kuzishirikisha Taasisi mbalimbali zinahusiana na masuala ya utawala bora kwa mara ya kwanza kukutana.
Taasisi hizo ni Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa, mamlaka ya kudhibiti manunuzi ya umma, na ofisi ya Taifa ya ukaguzi wa hesabu ambazo zilikuwa hazijawahi kukutana kufanya matembezi kama hayo nyingine ni Ofsi ya Rais,Utumishi na Utawala Bora,Tume ya Utumishi wa Umma na Tume ya Haki za Binadamu.
“Ipo mifano ya sehemu ambazo rushwa imekithiri kutokana na vitendoi vya rushwa na ufisadi. Kiongozi mkubwa anashindwa kumsimamia mtu aliyechini yake kama sheria ya maadili inavyomtaka kwasababu yeye mwenyewe mikono yake si misafi,” amesema na kuongeza kuwa , “matokeo yake hata mtu awe na mali nyingi, bado ataendelea kula rushwa bila kikomo”.
“Serikli ya awamu ya tano imedhamiria kupambana na rushwa ya aina zote kwa lengo la kujenga jamii yenye maadili inayochukia vitendo vya rushwa na ufisadi ili kuweza kuondoa rundo la rushwa ambalo lilikuwa limeanza kuikumba nchini kwa baadhi ya watumishi kujihusisha na masuala ya Rushwa.”amesema Balozi Kijazi
Kwa mujibu wa Balozi Kijazi, jitihada za serikali ni kuondokana na hulka ya ubinafsi na uroho na kujenga utamaduni na tabia ya kijitolea kwani hata awamu hii ya Rais Magufuli inapambana na janga hilo ndio maana kila Wizara imekuwa makini kwa watumishi wake na kuwaonya kuacha mara moja kujihusisha na Rushwa nchini
Aidha Katibu Mkuu Kiongozi ametoa wito kwa waandishi wa habari na vyombo vya habari kuonyesha uzalendo kwa kuielimisha jamii kuhusu maswala ya maadili nchini kwa kuandika ukweli wa mambo ili kuweza kufikisha ujumbe katika jamii zetu na kuunga mkono kauli hii ya kupiga Rushwa.
“Natoa wito kwa waandishi wa habari na vyombo vya habari kuonyesha uzalendo kwa taifa letu kwa kuielimisha jamii kuhusu kujenga, na kukuza maadili, haki za binadamu, uwajibikaji, utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa ili kuandika makala ambazo zinaonesha ukweli wa kuwaelimisha wananchi kwa nguvu zote na kuweza kuwa na jamii bora ambayo haina uroho wa Madaraka,” amesema.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna Valentino Mlowola ameeleza kuwa lengo la matembezi hayo ni kutuma ujumbe kwa wananchi kuhusu kujenga na kukuza maadili, haki za binadamu, uwajibikaji, utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa.
Kamishna Mlowola amesema, kuanzia Jumatatu ijayo, taasisi zinazohusika na masuala ya utawala bora zitakuwa na wiki ya utoaji huduma katika viwanja vya Mnazi Mmoja ili kupokea kero na malalamiko ya wananchi na kisha kuyashughulikia pamoja na kuyatatua kwa umakini kwa kufuata haki za kila binadamu ili aweze kusaidiwa ikiwa ana kero ambayo inamuumiza katika jamiii.
“Hii ni moja ya kampeini ya taasisi husika kuikataa rushwa, kujenga maadili na misingi ya uadilifu na kuhamasisha jamii kujua haki zao,” amesema.
Matembezi ya Leo ni ya mwendelezo wa Kampeni ya maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu ambayo yalifunguliwa Novemba 10 mwaka huu na yanatarajia kufikia kilele chake Desemba 10,2016 na pia amewataka watumishi waendelee kufanya mazoezi ili kujiweka fiti na sio kukomea siku ya Leo tu.