IGP Sirro Awapuuza wanasiasa wanao sema sema 'Kazi ndio Msingi'




WANASIASA nchini wametakiwa kuliacha jeshi la polisi lifanyekazi yake na kuwacha kulishinikiza kufanya kazi na kuombwa kutoa ushirikiano pindilinapo hitaji ushirikiano.

Kauli hiyo inatolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro jana, wakati akizungumza na waandishi wa hapari mkoani njombe ambapo amekuwa kwenye ziara ya kutembelea jeshi hilo kwa siku moja, na kusema kuwa wanasiasa wasilifundishe kazi jeshi hilo wakati akizungumzia kile wanacho endelea kuhusiana na tukio alilofanyiwa Tundu Lissu Mbunge wa Singida magraribu.

IGP Sirro alisema kuwa jeshi hilo linaendelea na kufanya uchunguzi wa tukio hilo na watawaambia watanzania walipo fikia kwa kuwa Jarada la tukio hilo badi wanalo na Wanasiasa hawawezi kuwafundisha watu wa kuwahiji wakati wao wanajua kazi yao.

“Wanasiasa kazi yao ni kuzungumza na wapiga kura wao wanataka kuwaona wanazungumza hiyo hawezi kuzuia wao kuzungumza kwa kuwa yeye anafanya kazi ya uchunguzi,” alisema IGP Sirro

Aidha Sirro alisema kuwa wanasiasa wanazungumza ili kuonekana na wapiga kula wao na wanakula posho kwa kuongea hivyo hata weza kuwazuia kuzingunza.

Alisema kuwa wanasiasa wanafanya siasa kwa kuwa kuna amani hivyo wamuache aendelee kufanya kazi yake ya kuhakikisha watanzania wanakuwa na amani, na kuwa amani iliyopo ikitoweka wanasiasa hawata fanya siasa wanazi fanya sasa.

“Wanasiasa wanazungumza kwa kuwa hapa nchini kuna amani waniache niendelee kufanya kazi yangu ya kuhakikisha kuna amani na wanasiasa wafanye siasa zao,” Alisema Sirro.

Pamoja na kupuuza maneno ya wanasiasa IGP Sirro amewataka wanajamii kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo hapa nchini kwa kutoa taarifa pale wanapo ona kuna uhitaji wa taarifa hizo na kwa watu wanao watilia shaka ili kukabiliana na watu wasio julikana wanao fanya matukio ya kinyama hapa nchini na kutokomea kusiko julikana.

Kauli hiyo ya Sirro inakuja baada ya kuwepo kwa maneo ya Ndugu wa Mbunge Tundu Lissu kulitaka jeshi hilo kuhakikisha uchunguzi juu ya tukio la kupigwa lisasi kwa Ndugu yao mjini Dodoma na kwenda kulazwa Nchini Kenya kwa matibabu.

Pamoja na sakata la Lissu Sirro ameataka wananchi mkoani njombe kuachanna na matukio ya kushirikia ambayo yanasababisha vifi kwa wanajamii wa mkoani humo huku akimuagiza kamanda wa Polisi mkoani humo hufanya vipindi vya kutoa elimu kwa wakazi wa mkoa huo juu ya madhara ya mauaji kwa imani hizo.

Alisema kuwa elimu ndio kitu pekee kinaweza kuondoa masuala ya mauaji ya imani za kishirikima bila imani jamii haiwezi kubadilika na kuachana na masuala hayo.