WADAU wa kupambana na
maambukizi mapya ya Ukimwi mkoa w anjombe wamesema kuwa kunachangamoto ya
baadhi ya watu kutoroka kupata dawa katika vituo vya kuchukulia dawa za
kupunguza makali ya Virusi vya Ukimwi.
Imedaiwa kuwa baadh ya watu wamekuwa wakitoroka kutoka katika
vituo vya kuchukulia dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi kwa
kushawishiwa na baadhi ya viongozi wa dini kuwa watawaombia na waache kuchukua
dawa hizo.
Wakizungumza katika mkutano wa wadau wa kupambana na virusi
vya ukimwi mkoa w anjombe unaojumuisha viongozi wa dini wa dini zote na
waratibu wa ukimwi mkoa na wilaya ya mkoa wa Njombe pamoja na wadau kutoka
asasi mbalimbali za kupambana na maambukizo ya virusi vya ukimwi.
Mmoja wa wadau hao kutoka taasisi za kidini Elias Msemwa wa
mkoani Njombe alisema kuwa kuna baadhi ya waumini wamekuwa wakikimbia dawa na
kwenda kwa baadhi wa viongozi wa dini kuombewa ambapo baada ya kuacha dawa hizo
asilimia kubwa ya hao hupotelea huko huko.
Alisema kuwa alifuatwa na muumini wake mmoja na kuambiwa kuwa
anataka kwenda katika kituo kimoja cha maombezi ambacho kina waambia wasinywe
dawa na watapona kitu ambacho hakukubaliana nachi na alimshauri muumini wake
kuhusiana na tukio hilo na kuomba watumishe wenzake kuto washawishi watu
kuachana na matumizi ya dawa.
Alisema kuwa baadhi ya watu wanao enda huko hupotelea huko
humo baada ya kuacha dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi, na
kusababisha watu hao kufa baada ya kuacha matumizi ya virusi vya Ukimwi.
Hata hivyo mratibu wa Ukimwi halmashauri ya Mji wa Njombe
(Chac), Daniel Mwasongwe, alisema kuwa katika halmashauri yake kuna watu ambao
wanakimbia katika vituo vya kuchukulia dawa na haijulikani kama wamefariki ama
bado wapo wanaishi.
“Halmshauri ya Njombe kuna watu 7662 wanatumia dawa, 3496
wamehama, 14 wamepotea, wamepotea, walio kimbia vituo vya kutolea dawa na
wameacha kunywa dawa hii ni hatari kwa kuwa haijulikani kama watu hao wamekufa
au wapo wanaishi,” alisema Mwasongwe.
Akiwasilisha tarifa ya halmashauri yake kuhusiana na
mapambano ya Ukimwi na utekelezaji wa mapambano ya ugongwa huo alisema kuwa
kuna watu, 18,460 Wanaoishi na virusi vya vya ukimwi halmashauri ya mji wa
Njombe na waliandishishwa katika vituo vya huduma, 7662 wanatumia dawa, 14
wamepotea, 3496 wamehama 1433 wamekufa.