Udongo mkoani Njombe Umepimbwa na wakulima kuanza kutumia mbolea sahihi kwa eneo husika



 Baadhi ya wakulima na wawakilishi wa vyama vya ushirika Njombe


BAADHI ya wa kulima mkoa wa Njombe wamedai kuwa kumekuwa na matokeo mabaya ya pembejeo za mazao waliyopanda ni kutokana na meneo hayo kupewa mbolea ambayo hairutubishi katika maeneo yao.

Licha ya kuwapo kwa changamoto hiyo iliyo ibuliwa katika semina kwa viongozi wa vyama vya ushirika vya msingi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huo, ambapo wakulima wanao hudumiwa na chama kikuu cha ushirika cha mkoa wa Njombe Njorecu walidai kupewa mbolea zisizo na matokeo mazuli katika maeneo yao kutokana na ubora a udongo wao kutofautiana kutoka eneo moja na lingine.

Chama kikuu cha ushirika mkoa wa Njombe kimeingia ubia na shirika la ujengaji wa uwezi wa kilimo vijijini la Briten ambapo limekuwa likiwasaidia kuwatafutia pembejeo mbalimbali za kilimo ambapo imedaiwa kuwa mbolea walizo patiwa kuto onyesha matokeo chanya na kukili kufanya barekebisho.

Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wamesema kuwa mbolea na mbegu walizo patiwa zilikuwa na matokeo yasiyo ridhisha na kuomba kuwa changamoto hizo zinatatuliwa kwa msimu ujao.

Akijibu matatizo hayo mtoa elimu kutoka taasisi ya Briten Ainea Mgulambwa alisema kuwa kwa mkoa wa Njombe kuta maeneo tofauti tofauti na aina za udongo ni tofauti na kuwa mbolea walizo kuwa wakizitoa kwa wakulima zilikuwa ni za aina moja kutokan ana kuwa haakua amefahamu changamoto ya kuapo kwa utofauti wa udongo.

Alisema kuwa kwa mkoa mzima a Njombe kumechukulia sampo za udongo kwaajili ya kwenda kupima udongo kitu kitakacho sababisha kila eneo kupatiwa mbolea kutokana na uhitaji wa udongo wa eneo husika.

Aliongeza kuwa taasisi hiyo msimu huu itahakikisha kuwa inatumia vipomo hivyo vya udongo wakati a kusambaza mbolea pamoja na kuhakikisha kuwa wananchi wanapata mbegu na kuwa mazao yao yanaongezeka.

Aidha aliwataka akulima licha ya kupatiwa mbolea kulingana na maeneo yao pia wahakikishe kuwa wanafuatilia kwa ukaribu wataalamu wa kilimo.

Mgulambwa aliongeza kuwa wananchi mbali ya kupanda kwa usahihi wahakikishe kuwa wanavuna kwa usahihi ili kupata mazao bora na kupata soko zuri na kuhakikisha kuwa mazao yao hayawi na takataka ili kuto sumbua sokoni.